CHAMA Cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA), kimeonesha nia yake ya kutaka kuwekeza katika mradi wa mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi huku ikiomba kufupishwa kwa masuala ya michakato katika kuingia ubia huo.
Tamstoa imeonyesha nia hiyo leo Ijumaa Novemba 22,2024 walipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Tanzania, David Kafulila, ambapo pamoja na mambo mengine walitaka kujua taratibu gani za kufuata ili kufanikisha hilo.
Wafanyabishara hao wanakuja na ombi hilo, wakati kukiwa na malalamiko ya uchache wa mabasi hayo jambo linalowafanya abiria kusubiri kwa muda mrefu vituoni.
Kwa upande wake Kafulila, amewaondoa hofu wafanyabiashara hao kuhusu michakato katika kuwekeza katika mradi huo kwa kile alichoeleza kumefanywa marekebisho ya sheria katika masuala ya ubia.
Social Plugin