Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imefanya vizuri kwenye Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafasi nchini (SHIMMUTA) yaliyofanyika mkoani Tanga kwa kutwaa vikombe viwili.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Meneja wa Kanda ya Kusini, Mhandisi Said Mkwawa, alitaja vikombe viwili ambavyo timu hiyo imeshinda kuwa kimoja ni cha mshindi wa kwanza kwenye mchezo wa drafti wa wanaume.
Alitaja kikombe cha pili ambacho timu hiyo imeibuka mshindi wa pili kuwa ni cha mchezo wa kuvuta kamba wanaume.
Mhandisi Mkwawa ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, alisema michezo hiyo ni muhimu kwa afya zetu za mwili na akili, lakini pia inawaleta pamoja kama wanamichezo na watumishi.
"Kwa hiyo pamoja na kushiriki michezo hiyo tukitafuta ushindi, imekuwa fursa nzuri ya kujenga afya zetu kupitia michezo," alisema Mhandisi Mkwawa.
Baadhi ya michezo ambayo ilishindaniwa kwenye mashindano hayo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, bao, ‘pooltable’, karata, riadha’na darts, kuvuta kamba, drafti na mingine.
Social Plugin