Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA ELIMU UDHIBITI UBORA KWENYE MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAWEKEZAJI WA ZABIBU


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wawekezaji wa Zabibu, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, mkoani Dodoma.

Katika maonesho hayo, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi (TBS) Bi. Sifa Chamgenzi ameeleza umuhimu wa viwango vya ubora katika bidhaa za zabibu, huku akielezea jukumu la TBS katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa nchini zinakidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya wananchi.

Elimu hii ililenga kuongeza ufahamu kuhusu udhibiti wa viwango, na kusaidia wananchi na wawekezaji katika sekta ya zabibu kuelewa mchango wa TBS katika kukuza uchumi na biashara za kimataifa.

Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi  (TBS) Bi. Sifa Chamgenzi, akitoa elimu ya masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wawekezaji wa Zabibu yanayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com