Mamlaka ya Mapato tanzania (TRA) yaibuka mshindi wa jumla kwenye uandaaji wa hesabu za kifedha zinazozingatia viwango vya kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) na Sekta za Kibiashara (IFRS). Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) jana 29/11/2024.
Vilevile, TRA imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories)kwenye tuzo hizo.
Akizungumza baada ya kupata tuzo hizo Naimbu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha amesema tuzo hizo ni uthibitisho wa dhamira ya TRA ya kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na weledi katika matumizi sahihi ya viwango vya juu vya kitaalamu katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa zake za kifedha.
Bw. Mcha ameongeza kuwa TRA inao watumishi wenye weledi wa kutosha katika usimamizi bora wa kifedha na uandaaji wa taarifa zinazozingatia viwango vya kimataifa. “Tuzo hizi ni uthibitisho kuwa TRA tunao watumishi wenye weledi katika kusimamia, kuandaa na kuwasilisha taarifa za fedha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa”.
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imekuwa ikiandaa tuzo kila mwaka kwa waandaaji wa taarifa za kifedha zinazozingatia viwango vya kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) na Sekta za Kibiashara (IFRS) ambapo tuzo za uwasilishaji wa taarifa za kifedha kwa mwaka 2023 zimetolewa jana tarehe 29.11.2024 APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Social Plugin