Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UDOM YANG'ARA TUZO ZA UANDAAJI BORA WA HESABU

 

Mkurugenzi wa Fedha CPA. Mwanjaa Lyezia akipokea tuzo toka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani (IAG), Bw. Benjamini Magai Katika ni Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA.Pius Maneno na kushoto ni Bw. Dickson wa Kurugenzi ya Uhasibu ya UDOM.

......

Chuo Kikuu cha Dodoma kimeibuka Mshindi wa Tatu katika kundi la Taasisi za Elimu ya Juu kwa uandaaji wa Hesabu bora kwa mwaka 2023.

Mafanikio hayo yanatokana na uandaaji bora wa hesabu za Taasisi kwa mwaka 2023 kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji Hesabu kwa Taasisi za Umma (IPSASs) ambapo Tuzo hizo huandaliwa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

Tuzo hizi zimetolewa tarehe 29 Novemba 2024 katika viwanja vya APC Bunju Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Taasisi Mbalimbali za Serikali.

Mgeni rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (IAG), Ndg. Benjamin Mashauri Magai.

Mkurugenzi wa Fedha CPA. Mwanjaa Lyezia akipokea tuzo toka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani (IAG), Bw. Benjamini Magai Katika ni Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA.Pius Maneno na kushoto ni Bw. Dickson wa Kurugenzi ya Uhasibu ya UDOM

Tuzo ya Mshindi wa Tatu UDOM

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule akishangilia ushindi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, baada ya kukabidhiwa Tuzo wakati wa halfa ya kutambua Taasisi zilizofanya vema katika uandaaji wa mahesabu kwa mwaka 2023 iliyofanyika Bunju jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Fedha UDOM CPA.Mwanjaa Lyezia,akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Malipo Bw. Dickson Hango mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya Mshindi wa Tatu katika Taasisi za Elimu, Ufungaji Bora wa Hesabu kwa mwaka 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com