Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ukiwa umeambatana na watumishi wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na watekelezaji wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar wamekitembelea Kikundi cha Ufugaji wa samaki kiitwacho UWASAMO, katika kata ya Mzinga Mtaa wa Konga Manispaa ya Morogoro, ili kuona mafanikio ya ufugajiwa samaki kwa wanakikundi baada ya kupata mafunzo ya Ufugaji samaki, biashara na utunzaji wa kumbukumbu kutoka kituo cha Kingolwira.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 6/11/2024 kwenye Kituo kinachojishughulisha na utoaji mafunzo ya ufugaji samaki, pamoja na uuzaji wa vifaranga vya samaki.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi ndugu Asungushe Patrick Msugupakulya amesema, wao kama kikundi wanaishukuru serika kwa kuwaletea mradi wa IFAD, ambao umewasaidia katika kuunda ushirika wao ambao mpaka sasa wanaendelea kupata msaada wa Elimu ya ufugaji wa samaki kwa wakati.
Pamoja na hayo wanakikundi cha UWASAMO, wamefurahishwa na ziara ya viongozi, ambapo wanaamini kwa kutembelewa huko, misaada zaidi watapata ili kuendeleza mtaji wao wa ufugaji wa samaki na kuleta maendeleo yenye tija kwa familia na Tanzania kwa ujumla wake.
Social Plugin