Hatimaye Filamu ya kuitangaza nchi Uchina ya “Amazing Tanzania” iliyomshirikisha Rais Samia Suluhu Hassan, Dr. Hussein Mwinyi na msanii Jin Dong kutoka China, imezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo Waziri wa Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amemwakilisha Rais Samia huku Serikali ya Uchina chini ya Rais Xi Jinping ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Utalii, Bw. Lu Yingchuan.
“Tayari tangu filamu hii izinduliwe Beijing Mei mwaka huu idadi ya watalii Wachina wanaokuja nchini imeongeza kutoka 44,000 mwaka jana hadi 54,000 kufika Septemba mwaka huu sawa na ongezeko la watalii 10,000 na bado mwaka wa utalii unaishia Disemba,” anasema Waziri Pindi Chana.
“Moja ya changamoto kubwa ni kuwa ‘location’ na viongozi wakubwa ni pamoja na muda wao kuwa mdogo na hata namna ya kumfanya kiongozi arudierudie kurekodi anapokuwa hajakamilisha vyema inaweza kuwa ngumu.
“Lakini timu zote tuliosimamia nao uzalishaji wa filamu hii na ile ya Royal Tour tunashukuru kuvuka vikwazo vyote hivyo,” ameeleza Dkt. Hassan Abbasi Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii aliyesimamia uzalishaji wa filamu hizo.
Social Plugin