WADAU WA MAENDELEO TANGA WAKUTANA DODOMA




Na Dotto Kwilasa,Dodoma.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa wamefanya kikao kazi cha kimkakati na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Wabunge wa Mkoa wa Tanga kwa lengo la kujadili mustakabali wa sekta ya maji na ujenzi kwa mkoa wa Tanga.

Akizungumza hivi karibuni katika kikao hicho jijini Dodoma Waziri wa maji Jumaa Aweso ameeleza kuwa mafanikio ya sekta ya maji Tanga yanahitaji ushirikiano wa wadau wote.

Aweso pia amewashukuru wabunge wa mkoa wa Tanga kwa upambanaji wao na kueleza kuwa siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri wa miradi ya kimkakati ndani ya mkoa huo.

"Jiji la Tanga linategemea mto Sigi na kutokana na mabadiliko ya tabianchi kina cha mto huo kinazidi kupungua, hivyo ni vyema tukaanza kutafakari sasa kwa maji yatakayofika Muhenza au Pangani yaweze kuelekezewa katika jiji la Tanga kwa kuwa jiji hilo ni la viwanda na matumizi ya maji ninmengi, "ameeleza.
Mbali na hayo Aweso amesema, " Hakuna asiyefahamu eneo la Mkata, zamani ukipita taswira ya Mkata pale yalikuwa ni madimbwi ya maji, tunatambua kabisa tulikuwa na mabwawa ya Manga yaliwekewa fedha zililiwa lakini matokeo hakuna, tulifanya kazi kubwa na nzuri hadi maji yamepatikana ambayo yanaweza kuhudumia wanamkata,"amesema

Waziri huyo mwenye dhamana ya maji pia ametumia kikao kazi hicho kumshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwezesha miradi mbali mbali mkoani Tanga hususani kwenye suala la Handeni na kueleza kuwa wananchi wataondokana na adha ya maji na kujikita kwenye shughuli za kiuchumi.

"Serikali imeongeza fedha nyingi kuwekeza Tanga, tumetoka Handeni tunakwenda katika wilaya nne na mradi zaidi wa bilioni 170 siyo jambo jepesi na miji inaenda kunufaika kwani fedha zipo na teki kubwa pale Handeni limekamilika.” amesema Awesoo

Pamoja na mambo mengine Aweso amesema wamefanya kikao cha viongozi wote wa chama na kuwapa mrejesho wa kazi ambayo inafanyika pamoja na kutuma timu ya wizara iliyopita kukagua miradi inayotekelezwa katika majimbo yote.

Amesema kuwa kazi ya mradi wa Handeni itatekelezwa usiku na mchana ili iweze kukamilika kwa wakati kwani fedha zimeshatengwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu Rajab Abdurahaman amesema mkoa wa Tanga umenufaika na maendeleo yatokanayo na kiwango kikubwa cha lami.

Amesema changamoto kwenye miradi ta barabara ni jambo ambalo lipo maeneo yote hivyo ni jambo ambalo halitamalizika kwa kipindi cha muda mfupi huku akitoa wito kwa wananchi wa Tanga kuwa wavumilivu.

"Tunaomba muwe wavumilivu, kwa mikakati ambayo Serikalini inafanya sisi tunaridhika nayo, tunaona kabisa tunakwenda kuufungua mkoa wetu wa Tanga irudi ile Tanga ambayo tunaijua sisi ikiongoza kiuchumi,” amesema Abdurahaman.

Amesema mafanikio ya sekta ya maji yanatokana na mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa sekta ya maji, wadau wa maendeleo, taasisi za fedha nje na ndani ya nchi.
“Kutokana na uzoefu na weledi nina Imani mtatoa maoni kwa mustakabali wa sekta hii miaka 25 ijayo,” amesema

Nao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho
ameeleza kuwa na imani na wizara ya maji na kwamba mipango ya wizara ya maji ni kuhakikisha inapeleka huduma ya maji maeneo muhimu ya uwekezaji ili kuendelea kuwavutia Wawekezaji.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ameeleza kuwa kazi kubwa pia ni kuhakikisha wananchi wa Tanga wanakuwa na uhakika wa maji ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji ili wavutiwe kuwekeza nchini.
Naye Waziri wa Ujenzi nchini Innocent Bashungwa amewahakikishia wadau hao wa maendeleo wa Tanga kuwa Serikali itaongeza bidii kuwekeza kwenye miundombinu ya barabara na maji iwe vizuri ili kuwarahisishia wawekezaji.

Aidha kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga na mjumbe wa kamati kuu ndugu Rajab Abdurahaman kimejumuisha wenyeviti wa CCM wa wilaya zote za Mkoa wa Tanga huku lengo na madhumuni ya kikao hicho ikiwa kujadili hali ya sekta ya maji na ujenzi kwa mkoa wa Tanga.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post