Na Danson Kaijage, DODOMA
WAFANYABIASHARA nchi wametakiwa kulipa kodi ya Serikali (VAT) kwa uaminifu kwa ili kuifanya serikali kufikia malengo yake ya kimaendeleo kama inavyokusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa na mchujagaji kiongozi wa kanisa la Calvary Assembles of God CAG,Mlima wa Nuru lililopo Chamelo Nzuguni 'B' Jijini Dodoma,Slvester Kamara alipokuwa akihubiri kanisani hapo juu ya umuhimu wa kutoa kodi kwa Serikali na Fungu la kumi la Mungu.
Mchungaji huyo katika mahubiri yake alisema kuwa ulipaji wa kodi kwa Serikali siyo suala la hiari bali ni maagizo ya Mungu mwenyewe kwani hata wakati wa Yesu kulikuwepo na utoaji wa kodi.
Kiongozi huyo wa Kiroho amezidi kusisitiza kuwa kitendo cha kutokulipa kodi ya Serikali au kutokutoa Zaka au fungu la kumi ni sawa na kutenda dhambi mbele za Mungu kuliibia taifa mapato yake.
Mchungqji Kamara alisema kuwa mfanyabiashara yoyote anayekwepa kulipa kodi au kutokulipa kodi kwa uaminifu ni wazi kuwa analifanya taifa kutokupiga hatua za kimaendeleo na kusababisha shughuli za maendeleo kuzorota.
"Kila mmoja anatambua kuwa kodi inayolipwa inachochea maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu,elimu,afya,Maji,Umeme pamoja na mambo mbalimbali ya kijamii.
"Hivyo basi ikitokea mtu akakwepa ulipaji wa Kodi itambulike wazi kuwa ni mwezi na anaenda kinyume na mpango wa Mungu kwani ikumbukwe kuwa hata Yesu alilipa kodi na kueleza wa zi kuwa cha Kaisali alipwe Kaisali na Cha Mungu alipwe Mungu"alisisitiza Mchungaji.
Akinukuu maandiko Mchungaji kamara alisema kuwa kitabu cha Mtakatifu Yohana sura ya 17 mstari wa 24 hadi 27 unaeleza haya "Mathayo 17:24-27
Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa.
"Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni?
"Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.
"Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza,na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli
,ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako"aliyasisitiza maandiko hayo.
Aidha Mchungaji alisema kuwa kitendo cha kutoa Zaka ni kumwibia Mungu na kujikosesha baraka hivyo ni wajibu kila mtu kutoa zaka.
Social Plugin