Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA WAKARIBISHWA KUJA KUJENGA VIWANDA TANZANIA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakijadiliana na Uongozi wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia, kuhusu fursa za ufanyaji biashara zilizopo Tanzania.

Na.Mwandishi Wetu-ETHIOPIA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka Mazingira bora na wezeshi yanayovutia wafanyabiashara kuja kuwekeza nchini hususani katika kuanzisha viwanda ili kutiumiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayolenga kujenga uchumi shindani na jumuishi wa viwand kwa lengo la kuongeza ajira na pato la Taifa .

Waziri jafo ameeasema hayo Novemba alipotembelea na kuzungumza na uongozi wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki (Eastern Industry Park) iliyopo Addis Ababa, Ethiopia yenye jumla ya viwanda takribani 257 ikiwemo viwanda vya chuma, nguo, na dawa na yenye nia ya kuja kuwekeza Tanzania kwa kujenga Kongani kubwa ya Viwanda.

Waziri Jafo akiwa ameambatana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina, Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia pamoja na wataalamu kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) utakaofanyika Novemba 9-10, 2024, mjini humo ameikaribisha kampuni hiyo na kuahidi kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Taasisi husika itaipa ushirikiano wa katika kuanzisha kongani hiyo.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki (Eastern Industry Park) Bi Ma Futao amesema Kampuni yake iko tayari kuwekeza Tanzania kwa kuwa mazingira ya ufanyaji biashara yanavutia ikiwemo Sera nzuri za biashara, bandari na miundombinu ya barabara na reli ya kisasa inayoinganisha na nchi jirani zisizo na bahari

Naye Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo amebainisha kuwa Kongani ya Viwanda ya Eastern ikijengwa Tanzania itaongeza ajira hususani kwa makundi maalum kama wananwake na vijana, pato la Taifa na hatimaye kukuza biashara na uchumi kwa ujumla.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) wakipeana mkono wa heri na Mmiki wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia Bw Bw.Lu Qixin mwenye nia ya kuwekeza Tanzania baada ya kutembelea Kongani hiyo ambapo amemkaribisha mwekezaji huyo kuja kuwekeza nchini ili kuongeza ujenzi wa Viwanda ambavyo vitatoa ajira nyingi kwa watanzania na kujenga uchumi wa nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakitembelea viwanda katika Kongani ya Eastern Industry iliyopo Addis Ababa, Ethiopia kujionea shughuli za uzalishaji kwa Mwekezajih uyo mwenye nia ya kuwekeza Tanzania.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakijadiliana na Uongozi wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia, kuhusu fursa za ufanyaji biashara zilizopo Tanzania.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo na ujumbe wa Tanzania amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unit Endüstri Makina Tekstil Ambalaj Tarım İthalat İhracat limited ya Uturuki Bw. Mustafa Albayram wa kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia ambapo Waziri Jafo amemukaribisha Mwekezaji huyo kuja kuwekeza na kufanya biashara nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Tirita General Trading ya Djibouti Bw. Abiy Araya kuhusu fursa za ufanyaji biashara Tanzania katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia ambapo Dkt. Abdallah amemukaribisha Mfanyabiashara huyo kuja kuwekeza na kufanya biashara nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com