Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKAZI ZAIDI YA 100 WA MAILIMOJA HADI VISIGA WAANZA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kibaha inaendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wakazi wa Mbwate, Kwa Mfipa, Simbani, Miembesaba, Uyaoni na Mailimoja. 

Pamoja na zoezi hilo, DAWASA Kibaha imetoa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasilino, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka. 

Wateja zaidi ya 100 wa maeneo tajwa wamepatiwa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi na zoezi hili ni endelevu. 

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0735 451 875 DAWASA - Kibaha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com