Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAHABARI DODOMA WANOLEWA KUHUSU M-MAMA



Na Happiness E. Chindiye,Habari - Dodoma RS

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Thomas Rutachunzibwa amefungua kikao kazi cha mafunzo ya mfumo wa huduma ya usafiri wa dharura ya mama mjamzito na mtoto mchanga (m-mama )kwa wanahabari wa Mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara.

Kikao kazi hicho cha siku moja kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Nashera Hoteli iliyopo Jijini Dodoma Oktoba 31,2024, lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa mfumo huo.

Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Rutachunzibwa ametoa wito kwa wanahabari kuendelea kutoa elimu kwa Umma juu ya suala la usafi kuwa ajenda ya kudumu, na uchukuaji wa tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com