Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAHARAKATI WALIA NA UKANDAMIZAJI WA HAKI YA MWANAMKE KWENYE SEKTA YA AFYA, UCHUMI NA UONGOZI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANAHARAKATI wa Jinsia na Maendeleo wameiomba Serikali kuingilia kati na kutatua changamoto zinazowakabili wanawake katika sekta ya afya, uchumi, na uongozi ikiwemo ukandamizaji wa haki kwa mwanamke.

Akizungumza leo,Novemba 13,2024 katika ofisi za Mtandao wa jinsia TGNP Mabibo-Jijini Dar es Salaam, Mwanaharakati wa jinsia na Maendeleo, Sharifa Hassan ameiomba serikali kudhibiti mianya ya Rushwa katika sekta ya afya ili kutimiza dhamira yake ya huduma bure kwa mama mjamzito na mtoto.

"Ukienda kujifungua unaambiwa ununue vifaa na hata kama vifaa ulibeba wanaacha vifaa vyako wanatumia vifaa vyao ilimradi tu utoe fedha"Amesema.

Amesema kumekuwa na huduma ambazo haziridhishi katika vituo vya kutoa huduma za afya katika maeneo mbalimbali huku wengi wakihitaji fedha ndo waweze kutoa huduma, jambo ambalo linakatisha tamaa

Aidha katika upande wa biashara amesisitiza serikali kulivalia njuga suala la mgawanyo wa meza kwani idadi ya wanaume wanaomiliki meza masokoni ni kubwa kuliko wanawake Jambo ambalo linahafisha juhudi za mwanamke katika kujiimarisha kiuchumi ambapo wanawake wengi wanapanga vitu vyao chini kwasababu ya kuukosa meza.

Pamoja na hayo Sharifa ameshauri kwamba ili kuwa na usawa katika uongozi inatakiwa kuundwe utaratibu ambao utasaidia uteuzi wa moja kwa moja kwa uwakilishi wa mwanamke katika uongozi kwa sababu wanawake wengi wanakwama kutokana na changamoto ya kiuchumi pamoja na Rushwa ya ngono.

Naye Mwanaharakati Mussa Abdallah ameeleza namna ambavyo mila kandamizi zinamnyima mwanamke nafasi ya kuimarika kiuchumi na kujikuta akifanya kazi nyingi kwa wakati mmoja kwa kipato hafifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com