NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WANAHARAKATI wa Jinsia na Maendeleo wameshauri kuwaunga mkono wanawake ambao wameteuliwa na vyama vyao kutokana na kukatwa majina ya wanawake wengi katika mchakato wa ndani wa vyama vyao.
Akizungumza jana Novemba 06,2024 Mabibo-Jjijini Dar es Salaam katika ofisi za Mtandao wa jinsia TGNP kwenye semina za jinsia na Maendeleo (GDSS)zinazofanyika kila Jumatano, Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Nobart Dotto amesema wao kama wanahaharakati wamedhamiria kwa dhati kuwaunga mkono wanawake walioteuliwa na vyama vyao kuanzia kipindi cha kampeni hadi katika kipindi cha kura.
Aidha Nobart ameeleza kuwa wanatamani kuona usawa wa kijinsia katika jamii ambapo wao kwa kuonesha dhamira ya nia yao wamewaahidi wagombea hao kuwaunga mkono katika kampeni pale zitakapo anza.
Kwa Upande wake ,Mwanaharakati wa Jinsia, Bi.Jackline Msafiri ameshauri wanawake ambao wameteuliwa na vyama vyao watambue kwamba hata kama wasipopitishwa, kura ndio zitakazo amua hivyo wawe wavumilivu.
Aidha Jackline amewaasa wanawake waliojitoa kugombea katika uongozi, majina yao yakikatwa katika awamu hii wasikate tamaa kwani hata yeye aliwahi kugombea awali lakini alipofikia katika hatua ya uteuzi alionekana hajakidhi sifa.