Na Dotto Kwilasa,Dodoma,Nov,17, 2024.
Mjumbe wa kamati ya siasa kata ya kilimani wilayani Dodoma amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani na mitaa yote minne kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wa kata ya kilimani kujitokeza kwa wengi ifikapo November 27 mwaka ili kuhakikisha wanatumia haki yao ya kikatiba kushiriki zoezi la kupiga kura kwa viongozi wao wa mitaa yote minne ya kata ya kilimani
Mjumbe huyo wa kamati ya siasa Comredi Barnabas kisengi ameyasema hayo wakati akizungimza na kituohichi kuelekea kuanza kwa kampeni ya vyama vya siasa kabla ya kufikia November 27 mwaka siku ya Uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.
"Tunakumbushana sisi kama wanachama wa chama cha Mapinduzi kuwa ifikapo November 20 hadi 26 vyama vyote tutakuwa kwenye mchakato wa kampeni za kuwanadi wagombea wetu waliteuliwa kuwania nafasi za Viongozi wa serikali za mitaa kwa nafasi ya wenyeviti na wajumbe wao watano katika mitaa yatu minne ya kilimani, Nyerere, chinyoyo na Image iliyopo katkika kata ya kilimani Jijini Dodoma '
Comredi Kisengi amesema kama wanachama wa CCM wakishikana kwa pamoja na kuhakikisha wanawanadi wagombea wao vizuri katika kampeni kueleza utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika mitaa yote minne kwa kipindi cha mwaka 2019 hadi 2024 hakika ilani ya CCM imetekelezeka kwa asilimia kubwa.
"Tunapaswa kuyasema yote mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi na kwa yaliyobaki basi wananchi watupe ridhaa yao tuweze kuyamalizia kwa kipindi hichi cha miaka mitano ijayo yani 2025 hadi 2030"amesema Comredi Kisengi
Aidha Comredi Kisengi amewataka wanacha kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu ambazo zitaleta tija ya ushindi wa kishindo kwa viongozi wao November 27 mwaka huu.
Amewasisitiza wanachama kuhakikisha wanajitokeza kuwahamasisha wanachi na wakereketwa wote waliojiandikisha kwenye daftari la makazi katika mitaa yao yote minne wajitokeze kwa wingi siku ya November 27 mwaka huu kupiga kura kwa kuwachagua Viongozi wetu wanapitia kutokana na chama cha Mapinduzi.
Aidha Comredi Kisengi amesema kuto kujitokeza kwenda kupiga kura ni kujikoseshea haki yako ya Msingi kumpata kiongozi wa mtaa wako hivyo wanachama na wananchi hakikisheni mnajitokeza siku hiyo ili uweze kumchagua kiongozi bora umtakaye atakayekusimamia maendeleo ya mtaa wako.