Na Mwandishi wetu,24 Novemba, 2024-Morogoro.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Mary Chatanda (MCC)* amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina imani kubwa sana na wanawake na kinaamini wanamchango mkubwa sana kwa maendeleo ya Taifa.
Chatanda amayasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Riverside, Kata ya Mwembesongo waliojitokeza kwenye kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hii leo.
Hata hivyo, Chatanda ameendelea na kampeni zake za Mtaa kwa Mtaa, Nyumba kwa Nyumba, Mguu Kwa Mguu huku akielezea mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Social Plugin