Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na (DAWASA) imekutana na kuzungumza na wateja wakubwa wa maji waliopo Wilaya ya Kinondoni na kuwasisitiza juu ya umuhimu wa wateja kulipa bili zao kwa wakati.
Zoezi hili linalenga kuwawezesha wateja hawa kutolimbikiza madeni kwa muda mrefu lakini pia kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma mara kwa mara.
Wateja wakubwa waliotembelewa ni pamoja na Protea Hotel, St. Joseph Cathedral High School, Big Joe Barbershop, CCBRT, CBE, Ubalozi wa Netherland na Ukumbi wa the Super Dome.
DAWASA inaendelea kuwasisitiza wananchi kulipa bili mapema ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na kutolipa kwa wakati.
Social Plugin