Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizungumza wakati akizindua Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
........
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kutengeneza mashine za kuchakata mwani na kukamua mafuta ya ufuta kwa wajasiliamali wa Mkoa wa Lindi walioko katika vikundi kwa kutumia Mfuko wa NEDF ili waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
Vilevile, ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kuhakikisha Wajasiliamali hao wanapata nembo ya ubora na "bar code" ili bidhaa zao ziweze kushindana katika soko la kimataifa kama EAC na AfCFTA.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo Novemba 02, 2024 alipokuwa akizindua Gulio la Bidhaa za Usindikaji, Ushonaji na Fursa za Biashara Mkoa wa Lindi linalofanyika kuanzia tarehe 01 hadi 03 Novemba 2024 Mkoani humo yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "ulipo ndipo walipoanzia".
Aidha, Waziri Jafo pia ameahidi kuwa Wizara yake itashirikiana na uongozi wa Mkoa huo katika kuweka mazingira bora ambayo yatawavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda kulingana na malighafi zinazopatikana katika mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Viwanda (2025- 2030) kwa lengo la kuongeza ajira na kukuza uchumi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kuusaidia Mkoa huo kupata Viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali ikiwemo mafuta ya Ufuta unaopatikana kwa wingi katika mkoa huo pamoja na viwanda vya kuchakata bidhaa za mwani .
Naye Mzee wa Kimila wa Mkoa wa Lindi Bw. Abdallah Hamis Livembe akimvisha vazi la Kimila la Utawala (Umwene) kama ishara ya mtawala wa Mkoa huo amemuomba Waziri Jafo kuipa Lindi kipaumnele katika kuanzisha Viwanda ili kuangeza ajira na kukuza uchumi wa Mkoa huo na kufuta jina la "Mkoa wa nyuma kimaendeleo".
Akizundua Soko Mtandao (e-Soko) katika Gulio hilo Waziri Jafo ameuelekeza Mkuu wa mkoa huo wa Lindi kuendesha Gulio hilo kila mwezi kwa kushirikiana na Tantrade na kulitangaza ili lifahamike na kuvutia wajasiliamali kwa kushiriki kuuza na kunua bidhaa mbalimbali huku akiwataka Watanzania kupenda kununua na kutumia bidhaa zinazotengenezwa nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) akivishwa vazi la kimila la umwinyi (Umwene) wa Mkoa wa Lindi na Mzee wa Kimila Mzee Abdallah Hamis Livembe kama ishara au Mtawala wa Mkoa huo wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiliamali kuona bidhaa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizungumza wakati akizindua Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(hayupo pichani), akizungumza wakati akizindua Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack,akizungumza wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
Social Plugin