Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Selemani Jafo (Mb), akishiriki Mkutano Maalum wa 45 wa Kisekta wa Viwanda, Biashara, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) Ngazi ya Mawaziri akiwa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Shaban Omary pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis L. Londo kujadili mapendekezo ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu kuboresha mazingira mazuri ya Biashara Novemba 15, 2024,Jijini Arusha.
Kikao hicho cha ngazi ya Mawaziri kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kimeongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Joseph Mum Majak.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Selemani Jafo (Mb), akimsikiliza Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya, Mhe. Salim Mvurya (wa kwanza kulia) baada ya Mkutano Maalum wa 45 wa Kisekta wa Viwanda, Biashara, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) Ngazi ya Mawaziri akiwa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Shaban Omary Novemba 15, 2024 Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, akiongoza kikao cha watalaam kabla ya Mkutano Maalum wa 45 wa Kisekta wa Viwanda, Biashara, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) Ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi kujadili mapendekezo ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu kuboresha mazingira ya Biashara Novemba 13, 2024,Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, akishiriki Mkutano Maalum wa 45 wa Kisekta wa Viwanda, Biashara, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) Ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi kujadili mapendekezo ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu kuboresha mazingira ya Biashara Novemba 13, 2024,Jijini Arusha.
Social Plugin