Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwa katika mkakati wa kuongeza idadi ya Waendesha Uchumi Walioidhinishwa (Authorized Economic Operators (AEO) ili kuongeza kasi ya uendeshaji wa shughuli za Uchumi nchini imekabidhi vyeti kwa Waendesha Uchumi watano ikiwemo Makampuni ya Jambo ( Jambo Group).
Zoezi la kuwakabidhi vyeti limefanywa mnamo Disemba 23, 2024 na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda na kupokelewa na Mkurugenzi mtendaji wa Makampuni ya Jambo, Khamis Salum Khamis na kuifanya Kampuni ya Jambo kuwa kati ya Waendesha Uchumi Walioidhinishwa (AEO) 41 waliopo nchini kwa sasa.
Kamishna wa TRA ameongeza kuwa Mapato ya mamlaka kwa asilimia zaidi ya 40 yanachangiwa na Bandari na kwa upande wa Bandari Waendesha Uchumi Walioidhinishwa wanachangia Asilimia zaidi ya 70 hivyo ni wadau muhimu kwa Uchumi wa nchi na kwamba TRA itahakikisha wanapata faida zote zinazotoka na kuidhinishwa kama ilivyo kwa wenzao waliopo nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Social Plugin