Tukio la kushtua limetokea mkoani Tabora, ambapo mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Petro Nasari, amekutwa amefariki dunia akiwa na mwanamke mmoja aitwaye Merysiana Edward, ambaye ni mke wa mtu.
Wawili hao wamekutwa wakiwa uchi wamegandana katika Stoo ya Grocery ya mzee Nasari, na wote walikuwa wamefariki.
Inaelezwa kuwa mke huyo wa mtu hakuonekana nyumbani kwake usiku ndipo ikabainika amefariki katika chumba kilichokuwa kinatumika kama stoo kwenye Grocery ya mwanaume huyo ambaye ni mmiliki wa grocery hiyo na mwanamke huyo ni mfanyakazi wa grocery hiyo.
Tukio hili limetokea jana katika mtaa wa Majengo, Kata ya Ipuli, ambapo miili ya marehemu hao iligunduliwa katika stoo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali unaendelea.
Ameongeza kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha vifo vyao.
Polisi wanachunguza tukio hili kwa undani zaidi, huku jamii ya Tabora ikishangazwa na hali hiyo
Social Plugin