Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini wamekutana na Wadau na Asasi za Kiraia zinazojihusisha na masuala ya afya na lishe mkoani Shinyanga kwa ajili ya kujadili masuala ya uboreshaji wa huduma za afya na lishe kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza Desemba 18, 2024 Mjini Shinyanga inatoa fursa ya kujadili changamoto na mafanikio katika masuala ya afya na lishe, na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, asasi za kiraia, na jamii kwa ujumla katika kuboresha huduma za afya na lishe, hasa kwa mama na mtoto.
Akizungumza katika warsha hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally, ameeleza furaha yake kutokana na hatua zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuzingatia na kuyapa kipaumbele masuala ya afya na lishe akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa dhati kutoka ngazi ya chini hadi juu ili kufikia malengo ya kuboresha afya na lishe.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally.
Amesema changamoto nyingi zinazohusiana na afya na lishe zinapatikana hasa kwenye ngazi za halmashauri, kata na vijiji, na kwamba mkoa wa Shinyanga una changamoto kubwa za ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni na ndoa za utotoni, ambazo zinahusiana moja kwa moja na afya na lishe za mama na mtoto.
Ally amesema upo umuhimu wa kuzingatia unyonyeshaji wa watoto, na kuwaomba akina mama na akina baba kuhamasisha masuala ya lishe bora, ikiwemo kutumia mama wakwe kama wadau wa kuhamasisha jamii ambao mara nyingi wamekuwa wakiwapangia waka mwana wao shughuli za kufanya badala ya kunyonyesha watoto hivyo kuathiri afya na lishe za watoto.
Ameongeza kuwa kazi kubwa inayohitajika ni kutekeleza mikakati iliyowekwa ili kuimarisha masuala ya afya na lishe, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na kuhamasisha familia na jamii katika masuala ya lishe na afya.
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson amesema lengo la mradi huo ni kuwafikia watu zaidi ya laki 1 na elfu 23 ili kuhakikisha wanaboresha Sera na Mazingira ya lishe kwa watoto wote pamoja na ushiriki wa wanafamilia katika masuala ya lishe
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson.
Shukrani ameelezea mikakati madhubuti ya shirika katika kuhamasisha jamii kuhusu lishe bora, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote katika kuboresha hali ya lishe, hususan kwa wanawake na watoto.
Amependekeza kuwahamasisha akina mama kunyonyesha watoto kwa wakati na kwa lishe bora ili kupambana na tatizo la udumavu.
Naye Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bagelela Kagiye Magana, amezungumza kuhusu mikakati ya sekta ya afya na sekta ya elimu ya kukabiliana na udumavu kwa watoto, ikiwemo uanzishwaji wa programu za lishe, ili kupunguza utapia mlo wa virutubisho na madini.
Kwa upande wake Afisa Lishe kutoka Wilaya ya Kishapu, Hadija Ahmed Nchakwi ameeleza hali ya lishe mkoani Shinyanga, ambapo udumavu ni asilimia 27.5, uzito pungufu ni 8.6%, na upungufu wa damu kwa watoto chini ya miaka mitano ni 69.7%.
Amebainisha mafanikio yaliyopatikana, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa kiwango cha utapiamlo mkali kutoka asilimia 32.1% mwaka 2018 hadi asilimia 27.5% mwaka 2021.
Amezitaja changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na ushiriki mdogo wa wanaume katika masuala ya lishe, mila na desturi za jamii, na uharibifu wa mazingira.
Ili kukabiliana na changamoto za utapiamlo na udumavu nchini wadau wa afya yakiwamo mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga yametakiwa kuunganisha nguvu pamoja ili kuwezesha upatikanaji wa lishe bora kwa jamii itayokayowezesha kufikia maendeleo endelevu.
Aidha Wadau hao kutoka asasi za kiraia wametoa mapendekezo kwa serikali, wakiomba kuwa viongozi wa dini, waganga wa kienyeji, na sungusungu wapewe elimu ili waweze kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya afya na lishe, na hivyo kusaidia kupunguza utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blogMkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMeneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka World Vision Tanzania, Shukrani Dickson unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Shinyanga Bi. Shukrani Dickson akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bagelela Kagiye Magana akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bagelela Kagiye Magana akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mtalaam wa Afya na Lishe kutoka World Vision Tanzania, Elizabeth Ndaba akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mtalaam wa Afya na Lishe kutoka World Vision Tanzania, Elizabeth Ndaba akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mtalaam wa Afya na Lishe kutoka World Vision Tanzania, Elizabeth Ndaba akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Bestina Gunje akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi kutoka TAMISEMI, Riziki Mbilinyi akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa ShinyangaMwakilishi kutoka TAMISEMI, Riziki Mbilinyi akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Afisa Lishe kutoka Wilaya ya Kishapu, Hadija Ahmed Nchakwi , akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau (Asasi za Kiraia) Mkoani Shinyanga yenye lengo la Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga Wadau wakipiga picha ya pamoja wakati wa warsha ya Kujadili Uboreshaji wa Huduma za Afya na Lishe mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin