Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAS SHINYANGA CP. SALUM HAMDUNI AAGIZA HALMASHAURI ZOTE KUTOA FEDHA ZA LISHE KWA WAKATI


Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamdun akizungumza  leo Alhamisi Desemba 19,2024 wakati akifungua rasmi Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP. Salum Hamduni, ameziagiza Halmashauri zote za Wilaya katika Mkoa wa Shinyanga kupitia Waganga Wakuu kuhakikisha fedha za utekelezaji wa shughuli za lishe zinatolewa kwa wakati, na kuendelea kusimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe, ikiwa ni pamoja na utoaji wa chakula shuleni. 

Agizo hilo amelitoa leo, Alhamisi, Desemba 19, 2024, wakati akifungua rasmi Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. Warsha hiyo imekusanya wadau na asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya lishe na afya ya mama na mtoto Mkoani Shinyanga.

Fedha za utekelezaji wa lishe bado hazijatolewa kwa wakati

CP. Hamduni amesema kwamba taarifa za utekelezaji wa mkataba wa lishe zinaonyesha kuwa fedha za kutekeleza afua za lishe zimepokelewa kwa asilimia 43 pekee. 

Ameeleza kuwa kati ya kiasi kilichopangwa cha shilingi 384,404,110/= kwa kipindi cha Juni 2024 hadi Desemba 17, 2024, kiasi cha shilingi 165,881,531/= kimetolewa, sawa na asilimia 43 tu. 

Hali hii, amesema, inaonyesha kutokuwepo kwa ufanisi katika utekelezaji wa shughuli hizo.

 "Nawaelekeza Halmashauri zote kupitia Waganga Wakuu kuhakikisha fedha za utekelezaji wa shughuli za lishe zinatolewa kwa wakati," amesisitiza CP. Hamduni.

Afua za lishe mkoani Shinyanga

Amesema kwamba, ingawa bado kuna changamoto, takwimu za lishe mkoani Shinyanga zinaonyesha mafanikio.

 Udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano umepungua kutoka asilimia 32.1 hadi asilimia 27.5, na ukondefu umeanguka kutoka asilimia 4.3 hadi 1.3. 

"Hii inaonesha kuwa juhudi zetu za kupambana na utapiamlo zinaanza kuzaa matunda. Hata hivyo, kiwango cha udumavu bado ni kikubwa, hivyo tunapaswa kuendelea kusimamia utekelezaji wa afua za lishe," amesema.

CP. Hamduni amelishukuru Shirika la World Vision kwa kushirikiana na Kivulini katika kusaidia Mkoa wa Shinyanga kutekeleza afua za lishe na afya ya mama na mtoto kupitia Mradi wa Grow Enrich na Nourish

Ameishukuru pia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa afua mbalimbali za afya, ikiwa ni pamoja na lishe na afya ya uzazi.

Shukrani Dickson

Mradi wa Grow Enrich na ushirikiano na wadau

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson, ameeleza kuwa shirika lake linashirikiana na serikali kutekeleza mradi wa miaka mitano, kuanzia mwaka 2023 hadi 2027, unaolenga kuimarisha hali ya afya na lishe kwa wavulana, wasichana, wanaume, na kukuza usawa wa kijinsia katika halmashauri za Wilaya ya Shinyanga na Kishapu. 

Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la World Vision Germany.

Yusuph Hamisi

Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Hamisi, amesema Mkoa umeendelea kushirikiana na wadau kupambana na utapiamlo, hasa kwa watoto chini ya miaka mitano, na kupunguza udumavu kwa kutoa elimu ya lishe kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha kupitia vituo vya afya.

Changamoto za mila na ushiriki wa wanaume

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally, amesema kwamba kikao hicho cha warsha kina na lengo la kutathmini utekelezaji wa afua za lishe, afya ya mama na mtoto, na kujadili mipango ya kuboresha huduma hizo mkoani Shinyanga.

Yasin Ally 

Amesema pia wanajadili utekelezaji wa ahadi za ukuaji wa afua za lishe zilizowekwa na serikali ya Tanzania kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo mwaka 2021.

Yasin ameeleza kuwa licha ya jitihada zinazofanywa, bado kuna changamoto ya ushiriki mdogo wa wanaume katika masuala ya lishe na afya ya mama na mtoto. 

Amesema kwamba ingawa wanaume wanashiriki katika kilimo, wakati wa mavuno, wengi wanauza mazao, kununua pombe, na kuoa wake wengine, hali inayochangia ugumu katika utekelezaji wa afua za lishe. 

Amesisitiza kuwa lazima kuwepo uhusiano kati ya ukatili wa kijinsia na lishe, na kuongeza umuhimu wa kuwaelimisha wanaume kuhusu mchango wao katika masuala haya.

Aidha, Yasin ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele cha kipekee masuala ya lishe na afya ya mama na mtoto, na kwa juhudi kubwa zinazochukuliwa kuboresha sekta hizi muhimu.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP. Salum Hamdun akizungumza  leo Alhamisi Desemba 19,2024 wakati akifungua rasmi Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP. Salum Hamdun akizungumza  leo Alhamisi Desemba 19,2024 wakati akifungua rasmi Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. 
 Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson, akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. 
Meneja wa Mradi wa Grow Enrich kutoka Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson, akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto, iliyoandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini. 
Mwakilishi kutoka TAMISEMI, Riziki Mbilinyi akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Bestina Gunje akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto
Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bagelela Kagiye Magana akizungumza wakati wa Warsha ya Siku mbili ya kutathmini uboreshaji wa huduma za lishe kwa afya ya mama na mtoto

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com