Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MNARANI BINGWA KOMBE LA MAIN FM

Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashidi Chuachua akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Mnarani FC ambao waliibuka mabingwa wa kombe la Main FM
Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashidi Chuachua akikabidhi mfano wa hundi kwa nahodha wa timu ya Mnarani FC ambao waliibuka washindi wa kombe la Main FM
Masudi William Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Main FM akizungumza wakati wa kuhitimisha mashindano ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na kituo hicho cha Radio.

Na Editha Karlo,Kigoma

TIMU ya soka ya Mnarani Bodaboda FC ya mjini Kigoma imeibuka mabingwa wa kombe la Main FC lililoshirikisha timu 20 za waendesha pikipiki maarufu bodaboda na hivyo kunyakua kitita cha shilingi milioni moja ikiwa ni zawadi kwa mabingwa wa mashindano hayo.

Mnarani ilifanikiwa kubeba ubingwa huo kwa kuifunga timu ya bodaboda Mlole kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma ambapo Mshindi wa Pili Mlole FC aliondoka na zawadi ya pesa taslim shilingi 500,000.

Aidha pamoja washindi kuondoka na fedha taslim pia wachezaji aliondoka viongozi wa timu zote mbili kila mmoja aliondoka na mtungi wa kilo sita wa gezi safi ya kupikia kutoka kampuni ya Oryx.
 
Akifunga mashindano hayo Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashidi Chuachua alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa na tija kubwa katika kufanikisha malengo yake kuhusu masuala ya afya lakini pia suala la nishati na gesi safi ya kupikia kuunga mkono Mpango wa Raisi Samia Suluhu Hassan wa kutaka kila Mtanzania kutumia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza katika kuhitimisha mashindano hayo Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Main FM cha mjini Kigoma, Masudi William alisema kuwa wamefanikiwa kutimiza lengo la mashindano hayo ya kwanza ya Main FM Cup ambayo mpango ni kuendelea katika kuibua vipaji na kufikisha ujumbe mbalimbali kwa jamii.

William alisema kuwa kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma na Ofisi ya Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani walikusudia kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu elimu ya afya ya uzazi na elimu ya usalama barabarani ambapo Oryx pia waliunga mkono mpango huo kwa kuja na mpango wa matumizi ya gesi safi ya kupikia.

Baadhi wananchi wapenda Soka wa Mkoa wa Kigoma wamekipongeza kituo cha redio cha Main FM kwa kuleta Ligi hiyo kwani wameweza kupata burudani.

“Niupongeze uongozi wa Radio ya Main FM kwakweli wamefanya kitu kizuri sana pamoja na kutupa burudani pia wanaibua vipaji vya watoto wetu”, alisema Abeid Ally mkazi wa Ujiji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com