Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wafanyabiashara mkoani Shinyanga wameonesha kuridhika na utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kupongeza jinsi inavyohamasisha na kuwezesha walipa kodi kulipa kodi kwa hiari, kinyume na hali ilivyokuwa hapo awali.
Pongezi hizo zimetolewa leo, Jumatatu Desemba 16, 2024, wakati wa ziara ya Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA akiwemo Meneja Msaidizi Huduma ya Mlipa Kodi Ramadhan Sengo katika makampuni ya GAKI Transporters Ltd (GAKI Investment Ltd na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) na Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd kwa ajili ya kuwashukuru kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati pamoja na kusikiliza kero na kupokea maoni.
Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo, ameeleza furaha yake kuhusu ushirikiano wa karibu wa TRA na wafanyabiashara, akisema kuwa hali ya sasa ni tofauti kubwa na ilivyokuwa awali.
Kileo amesema kwa sasa, wafanyabiashara wanapata elimu na msaada kuhusu masuala ya kodi, na kwamba TRA inahamasisha walipa kodi kutimiza wajibu wao bila shinikizo.
"Tunawashukuru sana TRA kwa kuendelea kuwa karibu na wafanyabiashara, Kimsingi TRA hivi sasa mpo vizuri, huduma kwa wateja ni nzuri, tofauti ni kubwa sana kwa sababu TRA ya sasa siyo ile ya kule tulikotoka. Sasa hivi tunalipa kodi kwa hiari, ule msukumano haupo tena. Naomba ushirikiano huu uendelee kuwepo ili tuendelee kujenga uchumi wa taifa letu",amesema.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Gilitu Enterprises Ltd, Gilitu Makula, amesisitiza umuhimu wa kulipa kodi kama njia ya kuhalalisha biashara na kuchangia maendeleo ya taifa.
Makula ameeleza kuwa utendaji wa TRA wa sasa ni wa mfano, kwani wafanyabiashara wanapata maelezo ya kina kuhusu utunzaji wa kumbukumbu na ulipaji wa kodi kwa usahihi.
"Mimi ni Mwekezaji mzawa, Mtanzania ninajivunia kuwa mlipaji kodi mzuri wa kodi kwa sababu bila kodi hatuwezi kuendelea kama nchi. Na ili uwekezaji wangu uwe halali ni muhimu kulipa kodi kwa sababu kodi inahalalisha biashara ”,ameeleza.
"TRA ya miaka ya sasa inatutembelea wafanyabiashara, inatuelimisha kuhusu masuala ya kodi na utunzaji wa kumbukumbu za malipo na kulipa kodi inayostahili. Noamba tulipe kodi kwa usahihi, na tuelimishane kuhusu umuhimu wa kodi," ameongeza Makula.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, ameshukuru wafanyabiashara kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati, akisisitiza kwamba mchango wao ni muhimu katika maendeleo ya taifa.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (katikati), na maafisa wengine wa TRA wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo
Maro amewahimiza wafanyabiashara wote kuwa mabalozi wazuri wa kodi na kutunza kumbukumbu za malipo, huku akiwashauri kutumia mashine za EFDs kwa ufanisi zaidi.
"Napenda kuwakumbusha walipa kodi kwamba muda wa kulipa kodi ya awamu nne kwa mwaka 2024 umewadia. Mlipa kodi lipa kodi yako mapema pamoja na madeni yako yote kuepukana na usumbufu. Ukiuza toa risiti, ukinunua dai risiti",ameongeza Maro.
Hii ni hatua kubwa katika kuboresha ushirikiano kati ya TRA na wafanyabiashara, ambapo sasa kuna mazingira ya kushirikiana, kujenga uelewa na kukuza ulipaji wa kodi kwa hiari, jambo linaloleta manufaa kwa pande zote na kwa taifa kwa ujumla.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kushoto) akizungumza alipotembelea Kampuni ya GAKI Transporters Ltd (GAKI Investment na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) leo Jumatatu Desemba 16,2024. Katikati ni Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (katikati) akizungumza alipotembelea Kampuni ya GAKI Transporters Ltd (GAKI Investment na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)
Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA akiwemo Meneja Msaidizi Huduma ya Mlipa Kodi Ramadhan Sengo walipotembelea kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo akimuongoza Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA kuangalia namna wanavyozalisha Vinywaji Vikali (Goldberg , Hanson's Lite, Diamond Rock na Hanson's Choice) katika kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, na maafisa wengine wa TRA wakiangalia namna uzalishalishaji wa Vinywaji Vikali (Goldberg , Hanson's Lite, Diamond Rock na Hanson's Choice) unavyofanyika katika kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (mwenye suti ya bluu) , na maafisa wengine wa TRA wakiangalia namna uzalishalishaji wa Vinywaji Vikali (Goldberg , Hanson's Lite, Diamond Rock na Hanson's Choice) unavyofanyika katika kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL)
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro akipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa GAKI Transporters Ltd, Gaspar Kileo (kushoto)
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula alipotembelea Kampuni hiyo
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro akizungumza alipotembelea Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (wa pili kushoto) akizungumza alipotembelea Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akizungumza wakati Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula (kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa wa TRA walipotembelea kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akielezea namna wanavyozalisha mafuta ya alizeti
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akiwatembeza maafisa wa TRA katika kiwanda cha uzalishaji mafuta
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akielezea namna wanavyozalisha mafuta ya alizeti
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa kutoka TRA wakiendelea kupata maelezo namna uzalishaji wa mafuta unavyofanyika
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro na maafisa kutoka TRA wakiondoka katika Mtambo wa Solvent unaokamua mafuta ya pamba katika kiwanda chake cha mafuta ya pamba na alizeti 'SANICO' kilichopo Mjini Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog