Na Hamisa Ally, Dodoma
Mwenyekiti wa mtaa wa chinyoyo kata ya Kilimani Mh Faustina Bendera amepiga marufuku wanachi wa Mtaa wake kuacha mara moja kuchota mchanga katika miundombinu ya barabara zote za mtaa wa chinyoyo kwakuwa ni uharibifu mkubwa wa barabara za mtaa.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kuona baadhi ya wanachi wakichota mchanga baada ya mvua kunyesha hivi karibuni
"Hivi karibuni baada ya mvua kunyesha kuna wananchi wameanza tabia ya kukusanya malundo ya mchanga katika barabara za mtaa Sasa ninawaambia ni marufuku kumwona mwananchi yoyote akisomba mchanga katika barabara za mtaa na yoyote tutakaye mkamata tutamkamata na kumchukulia hatua kali za kisheria ikiwa kupigwa fani na kupelekwa mahakamani"amesema Mwenyekiti Faustina
Aidha Mwenyekiti huyo amesema wanaotaka kusomba mchanga waende kwenye mtaro mkubwa unaujulikana kama mtaro wa wizara ya afya kwakuwa kuna mchanga unaoletwa na maji ya mvua pia watakuwa wamesaidia kuusafisha mtaro huo.
Mbalimbali na hilo mwenyekiti Faustina amewataadharisha wananchi katika kipindi hichi cha masika kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yao ya nyumbani na mtaani ili kuhakikisha wanaepukana na magonjwa ya kuharisha (kipindupindu) ambacho kwa tarifa zilizopita tayari kimeshabisha hodi jijini Dodoma naekusababiaha vifo.
Aidha Mwenyekiti Faustina amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya barabara zote za mtaa na kuwa wanatoa taarifa za maafa yoyote yatakayokuwa yanatokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha hapa Jiji Dodoma.
Social Plugin