Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM)CHA POKEA VITABU 200 VYA KUONGEZA UJUZI KUTOKA KAMPUNI YA CCCC KUTOKA CHINA


Makabidhiano ya Vitabu yakifanywa na  Mwakilishi wa Ubalozi wa China hapa nchini bwana Cha kun(Aliyevaa suti nyeusi) kwenda kwa Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Maktaba kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Collins Kimaryo (aliyevaa shati la batiki) katika Ukumbi wa Maktaba iliyopo Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

Na Hellen Kwavava..Dar es Salaam.
 
 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimepokea msaada wa vitabu 200 kutoka Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC), vitakavyoleta chachu ya kujisomea na kuongeza ujuzi pamoja na maarifa kwa wanafunzi.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya  vitabu hivyo iliyofanyika  jijini Dar es Salaam katika chuo hicho Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba chuoni hapo, Dkt. Collins Kimaryo amesema ni mara ya pili kupokea msaada wa vitabu kutoka Kampuni hiyo jambo ambalo linaleta furaha kuona wadau wanaunga mkono jihudi za usomaji wa vitabu.

Dkt. Kimaro amesema kuwa vitabu walivyopokea ni vya sanaa, historia, sayansi na teknolojia.

" Vitabu vinagusa sanaa, historia, sayansi na teknolojia. Vinatufaa maana kazi za msingi ni kutoa huduma za machapisho mbalimbali.

" Vitabu tunavyopokea vitaongeza maarifa kwa wanafunzi, vitaongeza aina za majarida tuliyonayo, pia kuonyesha ushirikiano baina ya China na Tanzania, pia Chuo Kikuu na Kampuni hiyo," amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo ya CCCC, Li Xuecai ni mara ya pili kugawa vitabu chuoni hapo ni ishara kwao inayoonyesha kuwa matukio  ni njia ya kuimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania na  pia ni sehemu ya kubadilishana utamduni baina ya nchi hizo mbili.

"Nashukuru kufikia tukio la kugawa vitabu kwa mara ya pili, mwaka jana pia tuligawa vitabu katika maktaba hii," amesema,

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtanzania Taasisi ya Confucius, Profesa Aldin Mutembei ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa nakala hizo 200 chuoni hapo.

Amesema  maktaba iliyopo chuoni hapo wanaifanya iendelea kujenga utamaduni baina ya Tanzania na China, pia kueleza watanzania namna gani China inaendelea.

Aidha  katika maktaba hiyo kuna vitabu Vinavyozungumzia utawala na mawazo ya China.

Hata hivyo amesisitiza kwa watanzania kutia juhudi katika usomaji wa vitabu kwani pia unasaidia kuchangamsha afya.
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Cha Kun akizungumza katika Hafla hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com