Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TEKNOLOJIA YA UHANDISI JENI (GMO) NI MKOMBOZI WA KUKUZA UCHUMI AFRIKA


Mtaalamu wa Masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Pius Yanda akizungumza na waandishi mara baada ya Kuwasilisha mada yake katika kongamano na Maonyesho ya Tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Kongamano hilo la siku tatu limeanza jana Desemba 2,2024 na litamalizika Desemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam
Mtaalamu wa Masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Pius Yanda akiwasilisha Mada yake mchango wa sayansi,teknolojia na ubunifu katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya nchi na kuchochea ubunifu katika baiteknolojia (GMO)

Na Hellen Kwavava - Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa Teknolojia ya Uhandisi jeni ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi,kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Sambamba na kupunguza kasi ya uzalishaji ya uzalishaji wa gesi joto afrika na duniani kwa ujumla.

Hayo  yamesemwa na Profesa Pius Yanda kutoka Taasisi ya usimamizi wa maliasili,mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchi iliyopo Chuo kikuu cha Dara es salaam (UDSM) Katika  Kongamano na maonyesho ya tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Profesa Yanda amesema katika mada yake kuhusu mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi aliweza kuelezea kuwa teknolojia hiyo ya Uhandisi Jes(GMO)imeanza kutumika  kwa kiasi kidogo kutokana na kutokuwa na teknolojia ya kutosha kuweza kutumia.

"Uhandisi jeni unatumika kwenye maeneo mengi ikiwemo elimu, afya, kilimo na maeneo mengine hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha kuna ubunifu wa ziada kutumia teknolojia hii kwa kiasi kikubwa," amesema. 

Aidha amesema kuwa ushirikiano na nchi zilizoendelea hususan katika utafiti, unaweza kuwa na ubunifu bora zaidi wa kukuza matumizi ya teknolojia hiyo kwa maendeleo ya Tanzania.

Amesema ubunifu wa ziada unahitajika ili kutumia rasilimali zilizopo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

"Mabadiliko ya tabia nchi yanatuathiri zaidi Afrika na Tanzania hivyo, suala la kutumia bayoteknolojia kwa ajili ya kutengeneza uchumi, ni vema kuboresha ikolojia kwa kuboresha maisha ya watu, kipato na kuchangia uchumi wa nchi,"amesema Yanda .

Kuhusu matumizi ya nishati safi, Profesa Yanda amesema Tanzania itakuwa mstari wa mbele katika matumizi ya nishati hiyo kwa kuhakikisha jamii inayoishi vijijini waweze kushiriki katika mkakati huo.

“Utashi wa kisiasa unaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan unaibeba Tanzania kuwa mstari wa mbele katika kuongeza matumizi ya nishati safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi",amesema 

Uhandisi Jeni ni teknolojia inayotumia michakato ya Kibaolojia  kuzalisha mbegu za Mazao na Mimea na ina sifa ya kukinzana na magonjwa,kustahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Mazao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com