Na: Lucas Magandula
Kauli ya Mh. Rais Dr. Samia Kuhusu Ukuaji wa Uchumi wa Kisasa na Shindani
Baada ya kuchukua uongozi wa taifa letu mwaka 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alianzisha mikakati mbalimbali ya kufungua njia za kiuchumi kupitia diplomasia ya uchumi.
Imani yake katika kukuza uchumi wa kisasa ni kujenga chumi zinazojumuisha na kuwezesha makundi yote ya kijamii, ikiwa ni pamoja na wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara wakubwa.
Hii imesaidia kuimarisha sekta ya utalii, ambapo takwimu za watalii zimeongezeka, na hivyo taifa limeendelea kupata fedha za kigeni.
Shabaha ya Ilani ya CCM ya 2020-2025 Kwenye Eneo la Uchumi
Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, ambayo ni mkataba kati ya wananchi na serikali, inalenga kukuza uchumi wa kisasa, jumuishi, na shindani. Huu unajengwa katika misingi ya viwanda, huduma za kiuchumi, na miundombinu wezeshi.
Maono ya Mbunge Katambi kwa Wanashinyanga Mjini Kuhusu Uchumi
Mh. Patrobas Katambi (Mb) anasema kwamba, licha ya utii na uaminifu wake kwa miongozo ya chama na mipango ya serikali, haijawahi kuwa na kipindi cha mafanikio makubwa kama hiki cha awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia.
Katika kipindi hiki, jimbo la Shinyanga mjini limepata fedha nyingi za ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya masoko na usafirishaji, ambazo zimewawezesha wajasiriamali kuwa na maeneo maalum ya kufanyia shughuli zao.
Hii inachochea ukuaji wa pato la taifa na kuboresha maisha ya wananchi. Wajasiriamali wanahamasika na kuona mabadiliko chanya katika uchumi wa jimbo lao.
Miradi ya Kiuchumi na Usafirishaji Iliyotekelezwa Jimbo la Shinyanga Mjini
Katika kipindi cha miaka minne (4) ya uongozi wa Dr. Samia, Mbunge Patrobas Katambi, na waheshimiwa madiwani, miradi ifuatayo imefanikiwa kutekelezwa:
- Soko kuu: Uboreshaji unaokamilika utagharimu Tshs bilioni 1.84
- Soko la Ngokolo Mitumbani: Uboreshaji umegharimu Tshs 500,000,000
- Soko la Ibinzamata: Uboreshaji umegharimu Tshs 620,000,000
- Soko la Mbogamboga Mnara wa Voda: Uboreshaji umegharimu Tshs 190,000,000
- Ukarabati wa Stendi ya Manyoni (Ibinzamata) pamoja na kuweka taa: Tshs 460,000,000
- Maboresho ya Stendi ya Soko kuu, Stendi ya Kambarage, maegesho ya magari, na soko la majengo mapya eneo la mapumziko NBC: Tshs 200,000,000
Hitimisho
Katika kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi wa Dr. Samia Suluhu Hassan, kazi kubwa imefanyika katika jimbo la Shinyanga. Shukrani ziende kwa Mh. Mbunge Katambi kwa juhudi zake katika kutafuta fedha za kukamilisha miradi hii mikubwa ya maendeleo. Waheshimiwa madiwani nao wanastahili pongezi kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazotokana na mapato ya ndani.
Aidha, pongezi za kipekee ziende kwa CCM kwa kuendelea kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. Tuendelee kumuunga mkono Mh. Rais na Mbunge ili waweze kutimiza mahitaji ya wananchi.
Shinyanga yetu, jukumu la maendeleo ni langu.
Social Plugin