Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MOTO WATEKETEZA ENEO LA BIASHARA YA VYAKULA NA VINYWAJI LA DILATI BUSTANI YA MANISPAA YA SONGEA



Na Regina Ndumbaro - Ruvuma 

MOTO umeunguza eneo la Biashara la Vyakula na Vinywaji liitwalo Dilati lililo ndani ya bustani ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma na kusababisha hasara ya kuteketeza vitu mbalimbali  ikiwemo Vinywaji ambavyo thamani yake hadi sasa bado haijajulikana.

 Akizungumzia tukio hilo Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Ruvuma Melenia Nyabwinyo  amesema tukio hilo limetokea Desemba 15 mwaka 2024 majira ya saa 4:00 asubuhi  hapo katika bustani ya Manispaa ya Songea .

Amefafanua kuwa taarifa hazikufika kwa wakati kwenye Jeshi hilo la zimamoto na Uokoaji licha ya kuwa baada ya kupatiwa taarifa hiyo mara moja Jeshi hilo likafika eneo la tukio na kuona moto umeshika kasi huku wakisema chanzo chake bado hakijajulikana.

Amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi majanga kama hayo yanapojitokeza kwenye maeneo yao.

Mmoja wa wafanyakazi katika eneo hilo Teresia Mwingira amesema wameshtushwa na moto huo na kuwa ulianzia eneo la jikoni ambako mhudumu mwenzao alikuwepo huko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com