• 4R katika Jimbo la Shinyanga Mjini zimevunja kambi za kisiasa na kupanda mbegu ya maendeleo kwa wananchi wote.
• 4R zimeleta mageuzi makubwa ya miradi ya maendeleo.
• 4R zimeleta uhusiano mzuri kati ya watendaji wa serikali, madiwani, mbunge na wananchi.
• 4R zimeondoa chuki na uhasama na zimeleta upendo, umoja, na mshikamano.
Na: Lucas Magandula
4R ZA DR. SAMIA SULUHU HASSAN
Miaka minne (4) ya uongozi na utawala wa Dr. Samia Suluhu Hassan umeongozwa na falsafa yake ya 4R, ikimaanisha uwepo wa Mageuzi, Ustahimilivu, Maridhiano, na Kujenga Upya. Kupitia falsafa hii, ndani ya kipindi hiki tumeshuhudia mageuzi na maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii, na kisiasa.
Hali ya demokrasia nchini inaendelea kukua, mshikamano na umoja wa kitaifa unaendelea kuimarika, na huku uhuru wa wananchi kutoa mawazo na uhuru wa vyombo vya habari ukiongezeka.
NUKUU YA BABA WA TAIFA
Aliwahi kusema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kuwa "Kazi ya uongozi sio kuwagawa watu, bali kazi halisi ya uongozi ni kuwajenga watu wawe kitu kimoja."
Kazi hii kubwa na njema katika miaka minne ya uongozi wa Mh. Patrobas Katambi amefanikisha kuwaunganisha watu na kuvunja kambi kubwa za kisiasa ambazo hapo awali zilikuwa zinasuguana, huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma muhimu za kijamii.
JICHO NA MAONO YA KATAMBI
Jicho na imani ya mbunge ni kwamba maendeleo ya Jimbo la Shinyanga Mjini hayawezi kupatikana wala kuletwa na mtu mwingine, bali sisi wenyewe. Kwa kuwa na umoja na mshikamano, ndiyo maana leo hii takribani ahadi zake zote za uchaguzi na ilani ya uchaguzi ametekeleza kwa kishindo, huku wananchi wakipunguza malalamiko ya ahadi hewa kama ilivyokuwa huko nyuma.
MAONI YA WADAU
Kwa kuwa siasa ni ushindani, leo hii ukiwasikiliza wakosoaji wa Mh. Mbunge Katambi, hawamkosoi kiongozi huyu kwa kushindwa kupeleka maendeleo kwa wananchi au ahadi hewa.
Katika eneo hili, wanakiri wazi kwamba kazi kubwa ndani ya miaka minne (4) imefanyika. Jimbo la Shinyanga Mjini limebadilika, na hata malalamiko ya wananchi juu ya kukosa huduma yamepungua. Wanachojivunia ni mbunge kuwa karibu zaidi na wananchi.
SIASA NI MAENDELEO
Wananchi kwa ujumla wao wanataka maendeleo, na ndio walichokichagua kwa Mh. Patrobas Katambi ambaye ndani ya miaka 4 ya uongozi wake, kwa kushirikiana na waheshimiwa madiwani na watendaji wa serikali, wamefanikisha kuleta neema na mafanikio makubwa. Maendeleo haya hata siku moja huwezi kuyatenganisha na juhudi na bidii ya Mh. Mbunge katika kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Rai yangu kwa wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini ni kuendelea kuunga mkono kazi njema za serikali ya awamu ya sita chini ya Dr. Samia, Mh. Mbunge, na madiwani wote, maana mtunda haya ni ahadi za uchaguzi na utekelezaji wa ilani ya CCM.
SHINYANGA YETU MAENDELEO JUKUMU LANGU
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin