Na Lydia Lugakila -Misenyi
Bi Amina ametoa kauli hiyo aliposhiriki siku ya maendeleo ya kata Bugandika (Bugandika day) ambapo alipata muda wa kushiriki maendeleo kwa kuahidi kiasi cha shilingi Milioni1 kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuleta maendeleo.
Amesema kuwa jitihada za Rais Samia ni kubwa sana kutokana na kubadilisha taratibu katika ufugaji wa Ng'ombe ambapo kwa sasa hakuna Mwananchi wa kawaida kumpa Ng'ombe, alafu kesho yake ukaja kumnyanganya badala yake unampa Ng'ombe anakulipa maziwa jambo alilolitaja kuwa limewapa ahueni ya maisha.
Ameongeza kuwa Rais Samia amefungua milango yote pembezoni mwa Nchi na fursa zimejaa hivyo kila Mwananchi ajipange kufaidi matunda ya Rais Samia kwani ni Mama mchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania.
Akieleza mpango huo wa kopa Ng'ombe lipa maziwa amesema benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Heifer international tayari wamehamasisha Wanawake na Wanaume kukubali kujiunga na ushirika kuendesha Biashara endelevu ya maziwa.
Amesema kupitia mpango huo unakopeshwa Ng'ombe unalipa maziwa ambapo kupitia Biashara ya maziwa hadi sasa wamesaini mkataba na msindikaji Kahama fresh Limited ambaye ndiye mnunuzi wa maziwa wanayozalisha.
"Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo makubwa Nchi nzima hivyo hatuna budi kuzidi kumuombea Rais wetu ili azidi kutufungulia milango zaidi",amesema Mwenyekiti huyo.
Bi Amina Ayubu ametumia fursa hiyo kuwaomba Wanawake na vijana Wilayani Misenyi kutobweteka kwani wanatakiwa kuelewa kuwa ufugaji ni fursa huku wakizingatia kuwa maisha ya sasa si mepesi.
"Wanawake tuamke najua ukiwa unavuna maziwa yako kwa siku unapata shilingi elfu 5 hadi elfu 10 watoto watasoma kila na kitu kitawezekana",amesema.
Ameongeza kuwa walisaini mkataba tangu Mwaka 2021 ambapo hadi sasa wapo wana ushirika wapatao 56 na wanatarajia kuboresha mradi huo kwa kuwa na kituo cha kupokelea maziwa kwani hadi sasa wanayasafirisha kutoka Bubale kwenda Bunazi ilipo ofisi ya msindikaji.
Aidha amesema wanajipanga kuwa na Ofisi yao na kuwa ujenzi wake umefikia hatua ya kupaua na ifikapo januari 10,2025 wataanza kupokea maziwa ndani ya Kijiji cha Bubale huku mratibu wa mradi huo Joseph Mabura kutoka jijini Dar es salaam akitarajia kufika katika kata ya Kakunyu Kijiji Bubale Wilayani Misenyi kwa ajili ya kukagua jengo hilo ifikapo Januari 7,2025.
Amempongeza mbunge wa jimbo la Nkenge Frolent Kyombo kwa kuwapa ushirikiano Wananchi Wilayani Misenyi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha katika miradi ya maendeleo huku akimuomba mbunge huyo kuwatengenezea barabara na kumuwezesha kujenga kituo cha kukusanya na kupoza maziwa Bubale.
Ametumia fursa hiyo kuwataka Wananchi walioko Jimbo la Nkenge kujiunga na mradi huo kupitia ushirika wa Bubale na ushirika wa maziwa Nsunga.
Social Plugin