Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Kampuni ya jambo group, imezindua kampeni ya Selebretika kijamukaya,kwa kuzalisha vinywaji vikiwa na chapa au Logo maalumu kwa ajili ya msimu wa sikukuu.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Desemba 21,2024 kwenye Ofisi za Jambo Media.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George, ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group, amesema, kampeni hiyo ya selebretika kijamukaya, ni kwa ajili ya wateja wao na watumiaji wote wa bidhaa za kampuni hiyo, kufurahia bidhaa za jambo wakiwa na familia zao katika msimu mzima wa sikukuu.
“Leo ni siku muhimu kwetu sisi makampuni ya jambo group, kwa sababu tunazindua kampeni yetu ya msimu wa sikukuu,Selebretika kijamukaya ambapo tumezalisha vinywaji maalumu vikiwa na chapa au logo kwa ajili ya msimu wa sikukuu na hii tumefanya ili kuleta radha nzuri ya kusheherekea kinyumbani zaidi,”amesema George.
“Ili nyumbani paweze kunoga na sikukuu iweze kuwa tamu zaidi unapo selebretika kijamukaya hakikisha nyumbani kwako kuanzia asubuhi mpaka jioni kuna kuwa na bidhaa za jambo, asubuhi ukiamka kuna vitafunwa vya jambo,maji ya jambo,juice za jambo, biskuti za jambo, Ice crem za jambo, na ukikosa vinywaji ya jambo kwenye meza yako sikukuu haiwezi kunoga,”ameongeza.
Pia, ametoa wito kwa wananchi wa kanda ya ziwa au mikoa yote ambayo bidhaa za jambo zinapatikana, na kwamba kama wameshidwa kufika nyumbani kufurahi na familia, watume hata katoni mbili za juice ya jambo dodo, soda, maji na mikate ya jambo, na ambao wanasafiri watumie bidhaa za jambo, ili waselebretike kijamukaya katika msimu huu wa sikukuu.
Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuona watu wote wanasheherekea sikukuu wakiwa na familia zao, na ambao watashindwa kujumuika kutokana na majukumu, basi wawapigie simu na kuwatakia heri ya Kristimas na mwaka mpya, pamoja na kutuma kitu chochote ili wafurahie,sababu familia ni sehemu ya kwanza ambayo inatengeneza msingi wa amani yako.
Aidha, ametumia pia fursa hiyo kutoa shukrani kwa wateja na watumiaji wa bidhaa za jambo, kwa kuwaungua mkono kwa mwaka mzima kutumia bidhaa za kampuni hiyo ambazo ni bidhaa bora kabisa.
TAZAMA PICHA 👇👇
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George, ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group,akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya Selebretika Kijamukaya na bidhaa za jambo msimu wa sikukuu.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George, ambaye pia ni kiongozi wa ubunifu na msimamizi wa chapa jambo group, akizundua Rasmi kampeni ya Selebretika kijamukaya na bidhaa za jambo msimu wa sikukuu.
Muonekano wa bidhaa za jambo zikiwa na chapa ya selebretika kijamukaya.
Picha zikipigwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya selebretika kijamukaya na bidhaa za jambo msimu wa sikukuu.
Social Plugin