Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YAWEKA HISTORIA ICC

 

Mtanzania Bi Glory Geofrey Sindilo amechaguliwa na Mkutano wa 23 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Roma (ASP-23) kuwa mjumbe wa Kamati ya Bajeti na Fedha (CBF) ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). 

Bi. Sindilo anakuwa Mtanzania wa kwanza kuchaguliwa katika Kamati hiyo muhimu ya kushauri Nchi Wanachama juu ya bajeti na masuala ya fedha ya ICC. 

Bi. Sindilo atahudumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia Januari 2025.

Bi. Sindilo ni Mtaalamu wa masula ya fedha aliye na usuli thabiti katika Uchumi, Fedha na Uhasibu. Ana uzoefu wa zaidi ya muongo mmoja katika Uhasibu wa kimataifa na utengamano wa kikanda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com