Mwili wa Mery Nassoro aliyefariki Desemba 5,2024 akiwa chumbani pamoja na mwanajeshi mstaafu, Petro Masali umezikwa leo kwenye makaburi ya Kanisa la Roman katoliki yaliyopo kata ya Ipuli manispaa ya Tabora bila misa ya msiba.
Katika hali ya kustaabisha watu wakiwa msibani mtaa wa Mhalitani wakiwa wamekusanyika wakatangaziwa kuwa hakutakuwa na ibaada wala wasifu wake, badala yake ataombewa sala tatu pekee kisha ataenda kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.
Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 7, 2024 Zakayo Gabriel kiongozi wa kanisa la Roman Katoliki, amesema kwa mujibu wa taratibu za kanisa Katoliki mtu anapofariki akiwa katika mazingira aliyokuwa nayo marehemu, anazikwa bila kufanyiwa ibada kama watu wengine.
"Tunasikitika kwamba marehemu hatafanyiwa ibada licha ya kwamba alikuwa muumini mzuri wa kanisa letu na kwenye jumuiya yetu, hivyo kwa mujibu wa maelekezo ambayo yametolewa na kanisa, ataombewa sala tatu pekee kisha ataenda kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele"
Aidha, kiongozi huyo ameeleza kuwa tukio lililotokea kwa muumini mwenzao liwe fundisho kwa wale wote ambao wanasaliti ndoa zao kwani kifo ni fumbo.
CHANZO - MWANANCHI
Social Plugin