Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wilayani Kahama.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanya Maadhimisho ya Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yenye kauli mbiu "Kuelekea miaka +30 Beijing chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia" katika Kata ya Nyihogo iliyopo Manispaa ya Kahama mkoani humo.
Katibu tawala Wilaya ya Kahama Hamad Mbega
Akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyka leo Desemba 06, 2024 katika Kata ya Nyihogo iliyopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga Katibu tawala Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega amesema lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu na kuikumbusha jamii kutoa taarifa za pindi wanapo baini uwepo wa vitendo vya ukatili katika maeneo yao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi amesema lengo la kuadhimisha maadhimisho hayo ni kuwakumbusha wazazi, walezi pamoja na watoto kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi sambamba na vyombo vingine ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili.
Naye Mstahiki meya Wilaya ya Kahama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyihogo Mhe. Sindano William amelipongeza jeshi la polisi kwa kuamua kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wakijinsia kwani imewakumbusha wazazi na walezi kutimiza jukulao na kushirikiana na jeshi la polisi katika mapambano ya vitendo vya ukatili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akiwaomba wananchi kushiriki katika mapambano ya vitendo vya ukatili wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kahama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akiwaomba wananchi kushiriki katika mapambano ya vitendo vya ukatili wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kahama.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akiwaomba wananchi kushiriki katika mapambano ya vitendo vya ukatili wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kahama.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akitoa ujumbe kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kahama.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Kamishina Msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Shuinyanga SACP Janeth Magomi amesema jeshi la polisi mkoani humo limeamua kuadhimisha siku hii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serikali katika mapambano ya vitendo vya uksatili wa kijinsia.
Social Plugin