Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, amechukua fomu rasmi ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo, Desemba 17, 2024, katika ofisi za makao makuu ya Chadema, Mikocheni, Dar es Salaam.
Sativa alimpigia simu Lissu jana, akimwambia kuwa anataka kumsaidia kwa sababu ana imani kwamba, endapo Lissu atafanikiwa kushinda nafasi ya uenyekiti, atahakikisha anahudumia masuala ya ukatili wa kijamii, hususan suala la watu kutekwa na kuuawa— jambo alilosema alilikutana nalo mwenyewe.
Lissu amedhamiria kuchukua nafasi ya Freeman Mbowe, ambaye amekuwa mwenyekiti wa Chadema kwa zaidi ya miaka 21 tangu mwaka 2003.
Uchaguzi wa viongozi wa Chadema unatarajiwa kufanyika Januari 21, 2025, ambapo Lissu atawania nafasi hiyo dhidi ya wanasiasa wengine kutoka ndani ya CHADEMA.
Social Plugin