Na Regina Ndumbaro - Ruvuma
Wamesema ingawa Mamlaka ya Udhibiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Kusini imepeleka wanyama katika bustani hiyo, bado kuna changamoto za miundombinu.
Wananchi wanaeleza kuwa kuboreshwa kwa miundombinu hiyo kutasaidia kujiingizia kipato kwa serikali na kuvutia watalii kutoka mikoa ya jirani.
Mkazi wa Mtaa wa Mshangano, Aidan Komba,amesema kuwa endapo bustani hiyo itaboreshwa kwa kuwekwa miundombinu bora, itakuwa chanzo kizuri cha mapato kwa serikali, hasa kutokana na watalii ,familia na watoto watakaotembelea eneo hilo.
Kwa upande wake, Agustino Nombo amesisitiza kuwa serikali inapaswa kuzingatia kuboresha miundombinu ya bustani hiyo ili kuhamasisha utalii wa ndani na kutoa fursa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma na majirani kutembelea.
Naye Aisha Abdalah, ameongeza kuwa ikiwa serikali itaongeza wanyama na kuboresha mazingira ya bustani hiyo kwa usafi na usalama, wananchi wengi watavutika kutembelea kama sehemu ya mapumziko ya kifamilia, hasa nyakati za sikukuu.
Social Plugin