Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Makoye Peter Mayala (45), mkazi wa kijiji cha Mwamagunguli kata Kolandoto Manispaa ya Shinyanga amejiua baada ya kumjeruhi mtoto wake mwenye umri wa miaka 6 kwa kumkata shingoni kwa kutumia kisu.
Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo, Desemba 2, 2024 katika kijiji cha Mwamagunguli kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga baada ya mwanaume huyo kutokuwa na maelewano na mkewe (jina linahifadhiwa).
Inaelezwa kuwa mkewe alikimbia nyumbani kutokana na mivutano ya kifamilia, na marehemu alichukua uamuzi wa kumjeruhi vibaya mtoto wake maeneo ya shingoni kabla ya kujinyonga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo