Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA BARA

 

Na Marco Maduhu SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga umeadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara,huku Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, akielezea mafanikio ya kimaendeleo ambayo yamefanyika mara baada ya nchi kupata uhuru mwaka 1961.

Maadhimisho hayo ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kimkoa yamefanyika leo Desemba 9,2024 katika Kata ya Salawe wilayani Shinyanga.
Mtatiro akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amesema kabla ya nchi kupata huru ilikuwa nyuma kimaendeleo, pamoja na ukosefu wa huduma mbalimbali za jamii.

Amesema baada ya nchi kupata uhuru, hadi sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo,huku pato la mwananchi katika Mkoa wa Shinyanga, likiongezeka na kufikia milioni 1.9 kwa mwaka.
Aidha,amesema mwaka 1961 katika sekta ya kilimo asilimia 75 ya wakulima walikuwa wakitumia zana duni, na hivyo kufanya kuwepo na uvunaji mdogo wa mavuno,lakini sasa hivi Tenknolojia imekua, na wakulima wamekuwa wakilima kisasa na kupata mavuno mengi.

Amesema mwaka 1961 Mkoa wa Shinyanga haukuwa na Viwanda Vikubwa na Kati, lakini baada ya kupata uhuru mwaka huo,hadi sasa kuna Viwanda Vikubwa 40,Kati 192,Vidogo 1,225.
Amesema kwa upande wa umeme hadi sasa vijiji 485 vina huduma hiyo,shule za awali na msingi 635 zimejengwa ambazo hazikuwepo, huku madarasa 1,663 yakijengwa pamoja na shule 15 za wanafunzi zenye ulemavu.

"Miaka hiyo hapa Shinyanga kulikuwa na shule moja tu ya Sekondari ambayo ni Shybush, lakini sasa hivi zipo shule 190 na nyingine 8 zinajengwa,"amesema Mtatiro.
Amesema katika sekta ya maji kulikuwa na visima 16,lakini sasa wananchi wa mjini wanapata maji asilimia 73 na vijijini asilimia 68,huku huduma za afya zikiongezeka,pamoja na upatikanaji wa majosho ya kuoshea mifugo 91 na marambo 54.

Katika hatua nyingine,amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu,huku akiwasisitiza pia kupanda miti pamoja na kufanya kilimo chenye tija.
Mtatiro pia amewasihi wananchi kupima afya zao mara kwa mara,pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) ili kujua afya zao.

Nao baadhi ya wazee akiwamo Benard Itendele na Spora Pangani,wamesema kabla ya nchi kupata uhuru watu walikuwa akiishi misiri ya wanyama chini ya wakoloni,lakini sasa hivi maisha ni mazuri na huduma zote za kijamii zinapatikana.
Katika maadhimisho hayo yalitanguliwa pia na zoezi la upandaji miti,upimaji wa virusi vya ukimwi,ushauri nasaha, pamoja na mpira wa miguu.

Kauli mbiu ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara inasema:Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 Benard Itendele akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 Sporah Pangani akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Silvester Mpemba akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yakiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akipima virusi vya ukimwi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akipokea majibu mara baada ya kupima virusi vya ukimwi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com