WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania Kanda ya Kaskazini (TFS) umetoa rai kwa watu waliovamia misitu ya Hifadhi kuondoka mara moja kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yao.
Alisema katika kuhakikisha wanalipa kipaumbele suala hilo wamejipanga kutumia teknolojia za kisasa na watatumia ndege nyuki (Drones) zitazo wasaidia kuangalia maeneo ya wavamizi na kuchukua hatua stahiki mapema.
Alisema kwa maana misitu mingine ni mikubwa sana na huko ndani kuna watu wanafanya kilimo cha madawa ya kulevya sasa kwa sababu ni ndani sana na watumishi ni wachache hivyo wakitumia teknolojia za kisasa hizo ili kuweza kuwaondoa .
“Nitoe rai kwa wavamizi wote waliopo kwenye misitu ya kanda ya kaskazi ikiwemo msitu wa hifadhi ya Bondo niwaambie Serikali itachukua hatua muda wowote kuanzia sasa hatutaweza kuvumilia muendelee kuteketeza misitu kwa maslahi yenu binafasi sio Tanga na maeneo yote kanda tutashirikiana na vyombo vyengine kuhakikisha tunawaondoa“Alisema
Aidha alisema misitu ni kwa ajili ya uhai na maisha na kila kitu kinachofanyika iwe ni nishati watanzania wengi wanategemea nishati inayotokana na misitu na sasa wanahamia kwenye kwenye nishati safi ambayo kwa maelekezo ya Rais itawasaidia kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu.
Kamanda huyo wa Kanda alisema pia kitu kingine ambacho kinachangia ni kilimo cha kuhama hama kwa maana wanapohama wanavyeka maeneo makubwa na kufungua maeneo mapya na kufanya hivyo wanaathiri uoto wa asili.
Awali akizungumza wakati akifunga kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Korogwe William Mwakilema alisema serikali inaendelea na mpango wake wa kuondoa wananchi waliovamia msitu wa bondo katika wilaya ya Kilindi na kufanya uharibifu kutokana na shughuli za kibinadamu wanazozifanya ikiwemo Kilimo,Ukataji Miti kwa ajili ya mkaa.
Social Plugin