Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MWENYEKITI WA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA PWANI, ALLY HENGO AFARIKI DUNIA

 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani, Ndugu Ally Hengo, amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa kutokana na majeraha ya ajali aliyoipata.

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani imethibitisha kifo hicho na inatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama wa klabu hiyo, na waandishi wa habari wote nchini.

Mipango ya maziko inaendelea, na taarifa zaidi zitatolewa.


R.I.P Ally Hengo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com