Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA CCCC YAAHIDI 2025 KUONGEZA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA


Meneja Msaidizi kutoka kampuni ya Ujenzi na mawasiliano ya China (CCCC) Li Yuliang akitoa neno wakati wa kikao kazi na Media katika hotel ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam

Msaidizi wa Ofisi ya Utawala toka CCCC akitoa Majumuisho ya majadiliano katika ya kampuni hiyo na Media

Na Hellen Kwavava -Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Ujenzi na mawasiliano ya China(CCCC) imesema Mwaka 2025 itaongeza na kuendeleza zaidi uhusiano bora na Vyombo vya habari nchini ili kukuza kazi pamoja na Uchumi wa nchi.

Meneja Msaidizi wa kampuni hiyo Li Yuliang ameyasema hayo wakati wa kikao kazi na vyombo vya habari vinavyojihusisha katika kuhabarisha umma kuhusiana na kazi mbalimbali zinazo fanywa na kampuni hiyo ya CCCC.

Akizungumza katika kikao kazi hicho Bwana Li amesema kuwa Mwaka 2025 watafanya jitihada katika kukuza ubora wa kutangaza kazi zao kupitia vyombo vya habari hivyo kikao hicho kimelenga kujua vitu gani waboreshe kama CCCC ili kupanua wigo wa kufikia jamii kubwa kupitia utangazaji.

“Kikao hiki cha kubadilisha mawazo kati yetu na nyinyi kutafanya kuleta mbinu mpya za ushirikiano kwa mwaka 2025 na jinsi ya kutekeleza vyema maoni yaliyotolewa”Alisema Li 

Aidha aliendelea kusema kuwa katika hatua nyingine tawi Lao hapa nchini linathamini sana fursa za kihistoria zilizopatikana kwa bidii na litakuwa mrithi mzuri,mjenzi na mtaalamu pamoja na kuendeleza ari kubwa ya uhusiano kati ya Taifa la china.

“Kampuni ya CCCC itafanya jitihada katika kufanya kazi hapa nchini kwa kuvutia na kuwaridhisha wateja pamoja na kuwa na uhusiano mzuri na jamii ya hapa nchini ili kukuza urafiki na uchumi kwa ujumla”

Kwa Upande wake Msaadizi wa Ofisi ya Utawala Yu Zixuan alisema kuwa wanatambua kuwa pamoja na maendeleo endelevu ya biashara yao katika soko la Tanzania wanafahamu kuwa vyombo vya habari ni kama daraja muhimu la usambazaji wa habari na lina jukumu muhimu katika kuunda taswira ya shirika na kuongeza ufahamu kwa umma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com