DAWASA NA K-WATER YA KOREA KUSHIRIKIANA NA KUBADILISHANA UZOEFU
Tuesday, December 10, 2024
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekusudia kufungua milango ya mashirikiano katika usimamizi wa Rasimali Maji na uendelezaji miundombinu ya Maji katika Sekta ya Maji ili kuboresha huduma za Maji Nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) akihitimisha ziara yake Nchini Seoul Korea alipokutana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya K-Water (Korea Water Resources Cooperation)
Dr. Yun Seog inayohusika na uendeshaji wa miundombinu ya maji, usimamizi wa rasilimali za maji, uzalisha na isambazaji wa Maji Korea.
Kupitia kikao hicho cha pamoja wamejadili mengi juu ya ishirikiano na Tanzania katika Sekta ya Maji na kukubaliana katika mikakati na mpango rasmi wa kufungua milango ya kufanya kazi pamoja na kwa kuanzia ni Mashirikiano kati ya K-WATER na Chuo cha Maji pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA).
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin