Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU KAZI AWAFUNDA WATUMISHI WA OSHA MASUALA YA KIUTENDAJI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga, akihutubia wakati wa kufunga kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA, pamoja mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 19, 2024.

*********************

Na Mwandishi Wetu

Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wametakiwa kuzingatia weledi katika kutekeleza jukumu lao la msingi la kusimamia usalama na afya mahali pa kazi ili kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma bora.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga, alipokuwa akifunga Kikao cha Tatu cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichohitimishwa jana (Desemba 19, 2024) Jijini Arusha.

Akiwasilisha hotuba yake ya kufunga kikao tajwa, Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, amesema kwakuzingatia wajibu wa OSHA wa kuzuia ajali, magonjwa na vifo mahali pa kazi, utekelezaji wa majukumu husika unahitaji weledi wa hali ya juu.

“Nitumie fursa hii kuwakumbusha kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia weledi, kuwa na nidhamu na kuepuka visingizio vya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku. Tukifanya kazi kwa weledi, tutaepuka kuwasababishia machungu zaidi wananchi tunaowahudumia ambao wakati mwignine wanakuwa wamekumbwa na matatizo kama vile ajali mahali pa kazi, kupoteza wapendwa wao au kuharibiwa mali zao,” amesema Katibu Mkuu.

Aidha, amewataka viongozi wa TUGHE na vyama vingine vya wafanyakazi kufanya jitihada kuzuia migogoro baina ya waajiri na wafanyakazi mahali pa kazi badala ya kusubiri kutatua migogoro inayotokea.

Awali, akimkaribisha Katibu Mkuu kufunga kikao, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa OSHA kilikuwa maalum kwa ajili ya kutathmini utendaji wa Taasisi kwa mwaka 2023/2024 pamoja na robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025.

“Kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi yetu ya mwaka fedha 2023/2024 na robo ya mwaka 2024/2025, tumefanikiwa kutimiza na hata kuvuka baadhi ya malengo yaliyopangwa na baraza hili jambo linaloashiria kwamba tunaenda vizuri,” amesema Bi. Mwenda.

Kwa upande wao Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Bw. Mudathir Athuman na mwakilishi wa wafanyakazi wa OSHA, Bw. Alfredy Shechambo, wameipongeza Menejimenti ya OSHA kwa kuandaa vikao vya mabaraza ya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria za nchi pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi yenye lengo la kuimarisha utendaji wao.

Mabazara ya Wafanyakazi nchini yapo kwa mujibu wa Waraka wa Rais Namba 1 wa mwaka 1970 uliowaelekeza waajiri kuwashirikisha wafanyakazi mahali pa kazi katika kupanga, kutekeleza na kutathimini matokeo ya kazi zinazofanyika.


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akiwasilisha salamu zake katika hafla ya kufunga kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18 na 19, 2024.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Taifa, Mudathir Athuman, akiwasilisha salamu za TUGHE katika hafla ya kufunga kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18 na 19, 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga akiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu (katikati) kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18 na 19, 2024. Alioambatana nao ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda (wapili kushoto) Mwezeshaji wa Mafunzo kwa watumishi, Bi. Martha Luleka (kushoto), Mwakilishi wa Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Mdathir Athuman (wapili kulia) na Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la OSHA, Bi. Beatrice Lengereri.

Wafanya kazi wa OSHA wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyo wasilishwa kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18 na kufuatiwa na mafunzo kwa watumishi wote Desemba 19, 2024. 

Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la OSHA, Beatrice Lengereri, akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18 na kufuatiwa na mafunzo kwa watumishi wote Desemba 19, 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga (kulia) akibadilishana mawazo na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18, 2024.

Mwezeshaji wa Mafunzo yaliyofanyika sambamba na kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA Jijini Arusha, Bi. Martha Luleka, akiwasilisha mada kuhusu ujuzi laini (Soft skills) katika kikao hicho.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga (katikati) na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Bw. Joshua Matiko (kulia), Mkurugenzi wa Mafunzo, Tafiti, Takwimu na Uhamasishaji na Dkt. Jerome Materu (kushoto), Mkurugenzi wa Usalama na Afya OSHA katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18, 2024 na kufuatiwa na mafunzo kwa watumishi wote Desemba 19, 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga (katikati) na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mameneja wa Kanda mbalimbali za OSHA katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18, 2024 na kufuatiwa na mafunzo kwa watumishi wote Desemba 19, 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga (katikati) na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na  watumishi tarajali wa OSHA katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Arusha Desemba 18, 2024 na kufuatiwa na mafunzo kwa watumishi wote Desemba 19, 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga akipokea zawadi kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. khadija Mwenda, mara baada ya kufunga kikao cha baraza la wafanyakazi wa OSHA pamoja na mafunzo kwa watumishi wote yaliyofanyika Jijini Arusha Desemba 18 na 19, 2024.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com