Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AKAGUA MAENDELEO UJENZI UWANJA WA NDEGE SHINYANGA ,AAGIZA UKAMILIKE APRIL 1,2025

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya  akizungumza wakati akikagua Maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga 
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati) akizungumza wakati akikagua Maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga 

Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amekagua maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli, uliopo katika Manispaa ya Shinyanga, na kuagiza  ujenzi wa uwanja huo ukamilike kwa wakati ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Shinyanga na mikoa jirani.

 Ziara hiyo imefanyika leo, Desemba 18, 2024, akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali.

Mhandisi Kasekenya amesema ameridhika na kasi ya ujenzi, na kusisitiza kwamba inapaswa kuendelea ili mradi ukamilike kabla ya Aprili 1, 2024."Nimeridhika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huu, hivyo niombe kasi ya ujenzi huu iendelee ili kufikia tarehe 1, Aprili 2024, ujenzi uwe umekamilika. Tutamuomba Mheshimiwa Rais Samia aje kutuzindulia uwanja huu ili uanze kutoa huduma kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani",amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha, Naibu Waziri Kasekenya ametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga , unaojengwa na Mkandarasi China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya shilingi 49,179,439,633.00/= pamoja na VAT na ukisimamiwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia kwa gharama ya Dola za Marekani 2,602,343 na Shilingi 23,735,554/= pamoja na VAT.

Amesisitiza kuwa uwanja huo utakuwa ni chachu ya maendeleo na kukuza uchumi mkoani Shinyanga.Mhandisi Fred Kipamila

Kwa upande mwingine, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Fred Kipamila, ambaye anasimamia mradi huo, ameeleza kwamba ujenzi wa uwanja umefikia kiwango kizuri, ambapo barabara ya ndege (Runway) tayari imekamilika.Gosberi Ruburi

Mhandisi mshauri wa mradi Gosberi Ruburi, amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa atasimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo ili ujenzi ukamilike kwa wakati na ndani ya muda wa mkataba, huku akiongeza kwamba serikali tayari imekwisha lipa fedha zote za mradi huo.

Tazama picha hapa chini👇

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati) akizungumza wakati akikagua Maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza akikagua Maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza akikagua Maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com