Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LGTI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KATIKA SAFARI YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI




Na Dotto Kwilasa,DODOMA

CHUO cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI)
kimejizatiti kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanapata kipaumbele nchini.

Katika kongamano la wanataaluma wa chuo hicho imejadiliwa mada ya matumizi ya nishati Safi, Changamoto Zilizopo na Uwezekano wa Kuhamasisha Wananchi kutumia nishati
mbadala ili kupunguza utegemezi wa nishati za kijenereta na umeme wa gridi hali itakayosaidia kwa kiasikikubwa kutunza mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la 16 la Wanazuoni lililofanyika katika Chuo hicho Kampasi Kuu ya Hombolo jijini Dodoma Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri, Prof. Magreth Bushesha, amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za chuo hicho kutoa mchango katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema, "Chuo chetu kimejizatiti kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya nishati safi kama vile nishati ya jua na upepo kwa ajili ya shughuli za kila siku,tunataka kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonyesha kuwa matumizi ya nishati mbadala ni suluhisho la kudumu kwa changamoto za nishati nchini, "amesisitiza

Profesa Bushesha ameeleza kuwa Serikali inahimiza matumizi ya nishati safi na mbadala kama sehemu ya sera yake ya kutunza mazingira na kukuza uchumi wa kijani hivyo kila mwanajamii anapaswa kuwa sehemu ya manadiliko hayo. LGT

Kwa upande wake Dkt. Kenneth Nzowa Mtaalamu Mwandamizi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania,ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi yana faida nyingi kwa jamii, uchumi, na mazingira na kufafanua kuwa Nishati safi, kama vile ya jua, upepo, na hidro, haina uchafuzi wa mazingira kama vile nishati za mafuta na makaa ya mawe.

" Hii inasaidia kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi zinazochangia mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza Gharama za Nishati ambapo baada ya uwekezaji wa awali, matumizi ya nishati safi kama nishati ya jua yanaweza kuwa na gharama za chini sana katika matumizi ya kila siku, kwani chanzo cha nishati (jua au upepo) hakihitaji gharama za kununua mafuta au malipo ya bili za umeme, "amesisitiza.

Amesema nishati safi inapatikana sehemu nyingi , na hivyo inawawezesha watu wengi, hasa katika maeneo ya vijijini, kupata nishati bora bila kutegemea miundombinu ya kitaifa ya umeme.

" Kuna faida nyingingi za nisahati mbadala kama kujenga Uchumi wa Kijani,Matumizi ya nishati safi husababisha kuongezeka kwa ujenzi wa miundombinu ya kijani, kama vile paneli za jua na mabomba ya upepo, na hivyo kuunda ajira mpya katika sekta za nishati na ujenzi, "amesema.

Ametaja faida nyingine kuwa ni Kuboresha Afya ya Jamii kwa kusaidia kupunguza uchafuzi wa hewa unaosababishwa na kutumia mafuta ambayo ni hatari kwa afya ambapo kupitia matumizi ya nishati mbadala, hali ya afya ya jamii inaweza kuboreshwa, hasa katika maeneo yaliyo na viwango vya uchafuzi wa hewa.

"Faida nyingine ni huondoa utegemezi mkubwa kwa vyanzo vya nishati vya nje, kama mafuta ya petroli au gesi, na hivyo kuongeza usalama wa nishati wa kitaifa,Nishati safi ni endelevu, maana yake inaweza kutumika kwa muda mrefu bila kupungua kwa wingi wake,kwa ujumla, matumizi ya nishati safi ni njia bora ya kudumisha maendeleo endelevu, kulinda mazingira, na kuboresha hali ya maisha ya jamii, "amesisitiza.

Hata hivyo Dkt. Nzowa ameishauri Serikali kuona namna ya kupunguza kodi kwenye viwanda vinavyo tengeneza nishati mbadala kama sola na gesi asilia ili kufanya nishati safi iweze kupatikana kwa urahisi zaidi na kwa wananchi wa hali za chini.

"Nasiaitiza umuhimu wa Serikali na wadau wa mazingingira kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida za nishati safi hususani maeneo ya vijijini ambako bado kuna uelewa mdogo kuhusu matumizi ya nishati safi.

"Ni muhimu kutoa elimu kwa watu ili waelewe jinsi nishati hii inavyoweza kuboresha maisha yao, kwa mfano, katika matumizi ya majiko ya gesi kwa kupikia na umwagiliaji wa mashamba kwa kutumia umeme, " amesema

Nate mmoja wa Mwanafunzi wa LGTI Fatuma Hassan, ameshauri uwepo wa Matumizi ya nishati safi kwenye shule na vyuo ili kuongeza ufanisi katika masomo ya wanafunzi kwani baadhi ya vyumba vya madarasa vimekuwa vikiathiriwa na kukosekana kwa umeme wa kutosha.

"Kwa kutumia nishati ya jua, tutaweza kuendelea na masomo yetu bila usumbufu wa umeme na pia tutakuwa tunatunza mazingira," amesema Fatuma.
















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com