Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHANDISI BWIRE AWAPONGEZA WALIOPANDISHA BENDERA MLIMA KILIMANJARO


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire, amekutana na kuwapongeza watumishi wa Mamlaka walioshiriki zoezi la kupandisha Bendera ya Taasisi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kusherekea miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.
Mhandisi Bwire amewataka watumishi wengine kutumia mafanikio hayo kama chachu ya kufanya vyema katika sehemu zao za kazi na kuisogeza Mamlaka katika mafanikio zaidi.

"Niwapongeze kwa mafanikio mliyoyapata, ni heshima kwa Taasisi, hii itumike kama chachu ya kufikia mafanikio ya jumla ya Mamlaka kwa kila mtumishi, zoezi hili likaonyeshe tija zaidi katika sehemu zenu za kazi," amesema Mhandisi Bwire.

Desemba 9, 2024 timu ya watumishi wa DAWASA walifanikiwa kufikisha Bendera ya Mamlaka katika kilele cha Mlima mrefu zaidi barani Afrika, Mlima Kilimanjaro zaidi ya mita 5,835 kutoka usawa wa bahari kusherekea miaka 63 ya Uhuru uliopatikana Desemba 9, 1961.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com