Mbunifu Ernest Maranya akionesha tuzo mbalimbali alizopewa Mbunifu katika kutambua Ujuzi wake na ubunifu.
Mbunifu Ernest Maranya akionesha tuzo mbalimbali alizopewa Mbunifu katika kutambua Ujuzi wake na ubunifu.
Na Hellen Kwavava - Dar wa Salaam.
Serikali imetakiwa kuangalia namna ya kuwepo kwa miongozo kwa ajili ya wagunduzi ili kuondoa changamoto iliyopo sasa ya kutokuwa na Muongozo.
Hayo ameyasema Mbunifu Ernest Maranya kutoka Taasisi ya Elimu ya Mafunzo ya Mafunzo ya Ufundi nchini (VETA) jijini Dar wa Salaam katika Maonyesho ya Tisa ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu (STICE)
Maranya alieleza kuwa ili kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wanaeleweka kisheria kuna kila sababu ya wadau wa elimu kuhakikisha wanakuwa na muongozo kwa ajili ya wabunifu.
Katika maonesho hayo Maranya ambaye amekuwa akionesha kifaa alichobuni kinachotoa elimu ya anga amesema pia ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuharakisha elimu ya anga kwa kutumia mfumo unaofanya kazi zaidi kukiwepo na Sumaku na ili utumike katika shule zote.
“Naiomba Serikali na wadau wa elimu nchini kuhakikisha wanaendelea kuniunga mkono katika kufanikisha ubunifu wangu unafika maeneo yote nchini.”Aliomba Maranya.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na kugundua mfumo huo na kukubalika lakini bado msukumo wa kuruhusu kuanza kutumia mashuleni bado ingawa anashukuru wadau wa elimu wamekuwa waliofika kwake kujifunza na kualikwa kwenye baadhi ya shule kuuelezea kwa wanafunzi.
Pamoja na mambo mengine Maranya amesema kuna shule za binafsi zaidi ya 30 ambazo ametembelea kutoa elimu hiyo lakini kunaugumu kwenye shule za serikali jwa sababu hakuna mwongozo wa kuzifikia shule.
Social Plugin