Na Mariam Kagenda_Kagera
Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Dkt. Abel Nyamahanga ameongoza matembezi ya amani yenye lengo la kusherekea kwa amani msimu wa sikukuu wa Krismas na Mwaka mpya.
Akiongoza matembezi hayo ambayo yamefanyika leo hi majira ya asubuhi katika uwanja wa Fatuma Muleba Mjini amewataka wananchi kusherekea kwa amani bila kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi chote cha sikukuu.
dkt. Nyamahanga amesema wamejipanga kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote wa msimu wa sikukuu na kusema kuwa Jeshi la Polisi halitosita kumchukulia hatua mtu yeyote ambaye atakayebainika akijihusisha na vitendo vya uharifu.
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mwl. Angasirini Kweka amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mazoezi ya viungo ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Kwa upande wake Afisa utamaduni na Michezo Wilaya ya Muleba Bw. Denis Joseph ametaja michezo iliyochezwa ambayo ni kuvuta kamba, kukimbia na limao kwa kutumia kijiko, mashindano ya kumenya ndizi pamoja na mazoezi ya viungo.
Social Plugin